Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zanzibar, Tanzania U-15 zatembeza kipigo Cecafa

Timu ya Taifa ya Zanzibar chini ya miaka 15 (U-15) na Timu ya taifa ya Tanzania Bara U-15 zimefanikiwa kupata ushindi katika mchezo wa pili wa mashindano ya Kombe la CECAFA kwa vijana wa umri wa miaka 15 yanayoendelea nchini Uganda.

Mchezo wa mapema uliochezwa saa 6:30 mchana uliwakutanisha Zanzibar U-15 dhidi ya Somalia katika Uwanja wa FUFA Technical Centre.

Zanzibar U-15 imeibuka kidedea kwa kupata ushindi wa mabao 4-0, mabao yaliyofungwa na Mohammed Salum Nassor akifunga moja kipindi cha kwanza.

Kipindi cha Pili Zanzibar U15 waliongeza kasi ya mchezo na kuongeza mabao matatu yaliyofungwa na Saleh Abdalla Mbarouk, Luqman Othman Omar na Hussain Ali Mbegu akashindilia msumari wa mwisho.

Saa 9:30 alasiri Tanzania Bara U-15 ilishuka dimbani kuivaa Rwanda mchezo ambao ulionekana kuwa wa kawaida kwa kukosa kasi kwa timu zote mbili.

Zikiwa dakika 45 za kipindi cha kwanza zinazidi kuyoyoma Peter Andrew aliwatoa kifua mbele Tanzania kwa kupata baomoja, mpaka timu hizo zinaenda mapumziko Tanzania Bara 1-0 Rwanda.

Kipindi cha Pili kilirudi kwa kasi na Timu kuanza kushambuliana kwa kasi na dakika ya 48 Peter Andrew alitikisa tena nyavu za Rwanda kwa kuwazawadia Tanzania Bara bao la pili huku bao la kufutia machozi la Rwanda limefungwa na Patrick Niyangabo dakika ya 89.

Matokeo hayo yanazifanya timu hizo kushinda michezo yote miwili waliyocheza huku Zanzibar U15 ikiwa haijarusu bao hata moja ikifunga mabao saba katika michezo hiyo na Tanzania Bara imeshinda michezo miwili ikifunga mabao matatu na kuruhusu baomoja.

Tanzania Bara na Zanzibar U15 zitakutana Jumamosi Novemba 11, 2023 saa 9:30 alasiri.