Zanzibar inaikaba koo bara hapa tu

Beki Boniface Maganga wa Kilimanjaro Stars akiwa na mpira akitaka kumpita
beki wa Zanzibar Heroes, Haji Mwinyi katika mchezo wa michuano ya Cecafa
jijini Nairobi, Kenya mwaka 2017. Katika mchezo huo Zanzibar Heroes iliibuka
na ushindi wa mabao 2-1. Picha|Maktaba
Muktasari:
Hata hivyo, kuna wachezaji wengine ambao wanakiwasha Bara ambao ni mtaji mkubwa kwao ndio maana mara nyingi Bara inapokutana na Zanzibar hufungwa kutokana na uwepo wa wachezaji wengi wanaotoka Bara akiwemo Aggrey Morris na Mwadin Ali (Azam FC), Juma Haji (Polisi Tanzania), Adil Nassoro, Abdalah Musa na Musa Haji (Mbao FC) na Seif Rashid (Lipuli FC).
WIKI mbili zilizopita kocha wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), Hemed Suleiman ‘Morocco’ alitangaza kikosi cha awali cha wachezaji 40, kitakachokwenda Kampala nchini Uganda kushiriki mashindano ya Cecafa yanayotarajiwa kuanza Desemba Mosi hadi 19, mwaka huu.
Katika kikosi hicho, wachezaji 17 wametoka Ligi Kuu Bara na waliosalia ni kutoka Visiwani. Waliotoka Bara ni Mohammed Abrahman (JKT TZ), Mohammed Muali (Polisi Tanzania), Abdallah Rashid ‘Babu’ (Ruvu Shooting) ambao ni viungo. Mabeki ni Mohammed Othman Mmanga (Polisi Tanzania, Abdallah Kheir (Azam), Ibrahim Ame Mohammed (Coastal Union) na Ally Ally (Yanga).
Viungo ni Abdul Aziz Makame (Yanga), Abdul swamad Kassim (Kagera), Awesu Awesu (Kagera), Mudathir Yahya (Azam), Kassim Suleiman (Azam), Feisal Salum (Yanga), Mohamed Issa (Yanga). Wengine ni Baraka Shaaban (Ruvu Shooting), Abdallah Hassan Nassor (Polisi Tanzania), Mohammed Mussa (Mbeya City) na Hassan Khamis (Azam FC).
Hata hivyo, kuna wachezaji wengine ambao wanakiwasha Bara ambao ni mtaji mkubwa kwao ndio maana mara nyingi Bara inapokutana na Zanzibar hufungwa kutokana na uwepo wa wachezaji wengi wanaotoka Bara akiwemo Aggrey Morris na Mwadin Ali (Azam FC), Juma Haji (Polisi Tanzania), Adil Nassoro, Abdalah Musa na Musa Haji (Mbao FC) na Seif Rashid (Lipuli FC).
KUHUSU BARA
Kilimanjaro Heroes inatarajiwa kuingia kambini baada ya michezo ya Ligi Kuu wikiendi hii kujiandaa na mashindano hayo, na timu hizo zinakutana kwenye kipute hicho ambacho mara nyingi Bara huchezea kichapo. Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila anasema ushindani hutokana na timu hizo kuwa na wachezaji wengi wanaocheza ligi moja, hivyo wanapopata nafasi hushindana ili kuzidi kupata nafasi kuitumikia nchi.
“Kupata namba kwenye timu ya taifa ni ngumu, hivyo mchezaji anapoitwa anaonyesha uwezo alionao na wachezaji hao hufahamiana ndio maana Bara hupata changamoto kubwa kwa kuwa wengi hucheza huku,” anasema Katwila.
Kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ anasema, “mara nyingi Zanzibar inapokutana na Bara hutaka kuonyesha ubora zaidi wakidai hutengwa ndio maana watatumia namna yoyote ili watufunge na sio mara moja wametufunga kwenye mashindano ambayo tunakutana nao.”
Katibu wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF), Mohammed Ali Hilal ‘Tedy’, anasema baada ya mazoezi ya siku nne Kocha Morocco alirudi Bara kuendelea na kazi na anatarajia kuanza rasmi kambi rasmi wiki ijayo baada ya wachezaji wote kuwasili.
MAKUNDI
Katika mashindano ya mwaka huu, Tanzania Bara ipo kundi C na Kenya, Djibouti pamoja na Zanzabar, na sasa inazifanya Bara na Zanzibar kusaka rekodi nyingine zitakapokutana kwani katika mchezo wa makundi 2017 uliofanyika Kenya, Bara ilichapwa 2-1 na Zanzibar ikatinga fainali na kufungwa kwa mikwaju ya penalti na Kenya baada dakika 90 kumalizika kwa sare ya 2-2.
Kundi ‘A’ ipo Uganda, Burundi, Ethiopia na Eritrea wakati kundi B kuna DRC Congo, Sudan, Sudan Kusini na Somalia.
TUJIKUMBUSHE
Katika mchezo wa mwisho timu hizo kwenye mashindano ya Cecafa, Bara ilifungwa 2-1 wakati ambapo timu hizo zilikuwa na vikosi ambavyo kwa sasa baadhi ya wachezaji wameendelea kuwepo.
Bara walikuwa: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Kennedy Juma, Kelvin Yondani, Abdallah Hamis, Shiza Kichuya, Himid Mao, Elias Maguri, Daniel Lyanga na Mzamiru Yassin.
Akiba: Peter Manyika, Boniphace Maganga, Mohammed Hussein, Jonas Mkude, Raphael Daud, Ibrahim Ajib, Abdul Hassan, Yahya Zaydi, Yohana Mkomola na Mbaraka Yussuf.
Zanzibar: Mohamed Abrahman, Ibrahim Mohamed, Haji Mwinyi Ngwali, Abdulla Kheri, Issa Haidar Dau, Abdul Azizi Makame, Mohamed Issa, Mudathir Yahya, Ibrahim Hamad Hilika, Feisal Salum na Hamad Mshamata,
Akiba: Ahmed Ali, Ibrahim Abdallah, Adeyum Saleh, Abdullah Haji, Seif Rashid (Karihe), Kassim Suleiman, Suleiman Kassim, Khamis Mussa, Amour Suleiman na Abdul Swamad Kassim.