Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ZA NDAANI KABISAA: Molinga, Chirwa kupigwa chini

HAKUNA namna, wajiandae tu. Ndio, washambuliaji wa zamani wa Yanga wanaokipiga Namungo kwa sasa, David Molinga ‘Falcao’ na Obrey Chirwa ni miongoni mwa wachezaji watakaotemwa na timu hiyo kutokana na kushindwa kuonyesha ubora.

Molinga hajafunga bao lolote hadi sasa wakati Namungo ikiwa imecheza mechi 19, wakati Chirwa amefunga mawili kitu kilichowashtua mabosi wao na kuanza kuwapigia hesabu kuwapiga chini mwishoni mwa msimu mikataba yao itakapoisha.

Mabosi wa Namungo waliamini majembe hayo yangeibeba timu hiyo hasa eneo la ushambuliaji, lakini wameshindwa kufanya mambo na kumkuachia mzigo Reliants Lusajo kuibeba timu.

Za Ndani Kabisa kutoka Namungo zinasema jamaa wanahesabiwa siku tu kabla ya kupewa mkono wa baibai.

Molinga alikiri kutokufunga bao hata moja kunamuumiza na anausikilizia uongozi kama utampa nafasi ama la, hali inayoelezwa ipo pia kwa Chirwa aliyetua akitokea Azam aliyojiunga nao baada ya awali kukipiga Yanga iliyomsajili toka FC Platinum ya Zimbabwe msimu wa 2015-2016.

Nyota hao walisajiliwa Namungo na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Hemed Morocco ambaye alijiondoa kutokana na mwenendo mbaya wa timu na nafasi yake kuchukuliwa kwa sasa na Mzambia Honour Janza anayesaidiwa na Jamhuri Kihwelo.