Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana waitwa kushiriki Kabaddi Zanzibar

KABADI Pict

Muktasari:

  • Kwa mwaka huu, Zanzibar itakuwa mwenyeji wa mashindano ya Afrika ya mchezo huo yatakayofanyika kuanzia Agosti 1 hadi 14.

MJUMBE wa Shirikisho la Mchezo wa Kabaddi Zanzibar, Abbas Khamis Suleiman, amewataka vijana kisiwani hapa kushiriki mchezo huo kwa lengo la kuzifikia fursa zilizopo.

Amesema, licha ya uchanga waliokuwa nao katika mchezo huo, lakini zipo baadhi ya timu zimeanza kuvutiwa na wachezaji wa mchezo huo ingawaje wanawaacha wakue ndipo wawaruhusu kutoka.

“Zanzibar ni timu changa lakini imeweza kutengeneza historia nzuri ya mchezo wa Kabaddi, hivyo natoa wito kwa vijana kujiunga kupata mafunzo ya mchezo huo kwa lengo la kuucheza,” alisema.

Alishauri kuwa watoto wanapaswa kufunzwa mchezo huo kuanzia shuleni ili usiwe na ugeni kwao kwani unajengwa kimwili na kiakili.

Mjumbe huyo aliwasihi wazazi wasitishike na mchezo huo kwa sababu Kabaddi ipo kisheria na ikitokea mchezaji kapata majeraha lazima apatiwe matibabu na stahiki zake.

Kwa mwaka huu, Zanzibar itakuwa mwenyeji wa mashindano ya Afrika ya mchezo huo yatakayofanyika kuanzia Agosti 1 hadi 14.