Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yondan awapiku mabeki wa Yanga

Beki wa timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam Kelvin Yondani. Picha na Maktaba

Muktasari:

Yondani aliifungia Yanga bao katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Ruvu juzi Jumapili. 

HATA Nadir Haroub, Oscar Joshua, Edward Charles, Juma Abdul wakija kupiga bao nyingi baadaye Kelvin Yondani atabaki kwenye rekodi kwamba ndiye beki wa kwanza kuifungia Yanga bao msimu huu.

Yondani aliifungia Yanga bao katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Ruvu juzi Jumapili.

Beki huyo anayejiamini amewaambia Simba kwamba atawasababishia matatizo makubwa watakapokutana na Yanga Oktoba 18 kwenye Uwanja wa Taifa na hata straika wao wanayemuamini, Emmanuel Okwi hataweza kufua dafu mbele yake achilia mbali mabeki wengine.

Yondani ambaye ni baba wa watoto wawili aliiambia Mwanaspoti kwamba: “Najua Simba inamtazama sana Okwi kwa sasa na ndiye watakayemtegemea kutufunga, haitakuwa rahisi hivyo, mimi nitamtuliza na kuhakikisha hafanyi chochote. Najua staili yake ya uchezaji.”

“Pia Simba wana kocha wao, Patrick Phiri, namuheshimu sana na ni kama baba yangu lakini kwasasa niko mbali na yeye na ninaamini mbinu ambazo aliwahi kunifundisha ndizo nitakazozitumia kuwaumiza na hii si kwasababu niko kwenye timu ya Yanga, ni kwasababu nahitaji heshima kwa kufanya kazi yangu inavyotakiwa na kumpa raha mwajiri wangu,” alisema Yondani.

Wachezaji wa Yanga, Haruna Niyonzima na Mrisho Ngassa wamezungumzia mchezo huo kwa tahadhari; “Tuko vizuri na tuna uwezo wa kupata ushindi kwenye mchezo wa Simba lakini hatuwabezi, licha ya kwamba hawajashinda mechi yoyote lakini bado wanacheza kwa kiwango cha kuridhisha, tusubiri dakika 90.”

Ngassa ambaye kwa sasa amekuwa akilaumiwa na kocha wa timu hiyo, Mbrazili Marcio Maximo kwa kucheza mpira wa kuremba alisema mchezo huo wa Simba utakuwa ni mgumu kuliko unavyotabiriwa hivyo watahitaji maandalizi ya ziada ili kupata matokeo.

“Tutaingia tukiwa tunajiamini zaidi hususani baada ya kushinda mara mbili mfululizo. Ila mchezo huo utakuwa mgumu, Simba watajaribu kufanya marekebisho na kuangalia walipokosea, watakuja na akili nyingine kabisa hivyo ni dhahiri kuwa shughuli itakuwa pevu,” alisema Ngassa.

Simba ilitoka sare ya mabao 2-2 na Coastal Union kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 na timu za Polisi Morogoro na Stand United, Yanga ilifungwa mabao 2-0 na Mtibwa Sugar kabla ya kuzifunga mabao 2-1 timu za Prisons na JKT Ruvu.