Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

YAS, Korosho Marathoni kuwabeba wakulima

KOLO Pict

Muktasari:

  • Peter aliibuka mshindi kwa upande wa wanaume na Cecilia alishinda kwa wanawake na kila mmoja kuzoa Sh 3.5 Milioni walizokabidhiwa katika hafla ya kufunga mbio hizo zilizofanyika leo katika viwanja vya Millenium Beach, mkoani humo.

MBIO za Korosho Marathoni 2025 zimefanyika wikiendi iliyopita, ikishuhudiwa Peter Gidoska na Cecilia Ginoka wakiibuka kidedea katika kilomita 21, huku kampuni ya Yas ikithibitisha kuendelea kushirikiana na waandaaji wa mbio hizo ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha wakulima wa korosho na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi mkoani Mtwara kupitia michezo. 

Peter aliibuka mshindi kwa upande wa wanaume na Cecilia alishinda kwa wanawake na kila mmoja kuzoa Sh 3.5 Milioni walizokabidhiwa katika hafla ya kufunga mbio hizo zilizofanyika leo katika viwanja vya Millenium Beach, mkoani humo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Maendeleo ya Vijana), Dk Joel Nanauka aliipongeza Yas kwa mchango wao wa kuboresha ustawi wa vijana, wakulima na jamii ya Mtwara. 

“Niwapongeze Yas kwa uwekezaji mkubwa mnaoufanya mkoani Mtwara, kuanzia miundombinu ya mawasiliano, huduma za kifedha kwa wakulima, hadi ushiriki wenu katika matukio kama Korosho Marathon," alisem Waziri Nanauka na kuongeza;

"Haya ni matokeo ya kampuni inayotazama mbali na inayotambua maendeleo ya taifa letu yanategemea uwezeshaji wa vijana, wakulima na familia zetu. Serikali itaendelea kushirikiana nanyi kuhakikisha wakulima wa korosho wanapata huduma bora, salama na za uhakika.”

KO 01
caption... WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Maendeleo ya Vijana), Dk Joel Nanauka (kulia) na Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Pwani Kusini, Fadhila Saidi (kushoto) wakikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi 1.5 Milioni kwa Enestina Mngolage baada ya kushika nafasi ya pili katika Mbio za Korosho Marathoni kilomita 10 kwa wanawake.

Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Pwani Kusini, Fadhila Saidi alisema ushiriki wa Yas na Mixx katika Korosho Marathon ni sehemu ya mkakati wa kampuni kuboresha maisha ya wakulima na jamii kupitia huduma bunifu za kidijitali, kifedha na kijamii.

"Ushirikiano na Bodi ya Korosho, AMCOS na vyama vikuu vya Ushirika kuwezesha malipo ya wakulima kupitia Mixx kwa haraka na kwa usalama zaidi.  Kuwezesha zaidi ya Shilingi 150 bilioni 150 kulipwa kwa wakulima zaidi ya laki moja tangu mwaka 2017," alisema Fadhila na kuongeza;

“Korosho Marathon sio tu tukio la michezo, bali ni jukwaa muhimu la kuutangaza mkoa wa Mtwara kimataifa, kukuza utalii, biashara, afya na umoja wa jamii. Ni ishara ya fahari ya wakulima na mchango wao katika uchumi wa Taifa.”

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Korosho Marathon, Nelson Mrashani, alimshukuru Dk Nanauka kwa kushirika katika mbio hizo na vilevile aliwapongeza washindi na kuwashukuru washirika wa mbio.

“Tunawashukuru sana washirika wetu na wakimbiaji wote kwa kuungana nasi katika juhudi za kuchochea Michezo, Afya na Biashara hapa Mtwara," alisema mwenyekiti wa mbio hizo zilizoshuhudia pia; Vaileth Adam  aliyeshika nafasi ya pili kwa wanawake na kuzoa Sh 2.5 milioni.

Mshindi wa tatu kwa wanawake alikuwa ni Natalia Sule aliyenyaku Sh 2 milioni, huku kwa Protas Kableni alishika nafasi ya pili kwa wanaume akitwaa Sh 2.5 milioni huku Dickson Paul  akiwa wa tatu.

Kwa mbio za kilomita 0, Grace Jackson Charles ndiye aliyeibuka kidedea akifuatiwa na Enestina Ngoloje na Deborah Benedict, huku Jumanne Mnada aking'ara kwa wanaume akifuatiwa na John Joseph na Shedrack Damas na kila mmoja kuzawadiwa kati ya Sh 2 milioni, Sh 1.5 milioni na Sh1 milioni kulingana na nafasi kwa jinsia zote.