Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yawaficha Mzimbabwe, Mtogo

Mchezaji wa Yanga, Thabani Kamusoko

Muktasari:

Simba ipo Zanzibar kwa kambi ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara msimu ujao, lakini uwepo wao umefuta ratiba ya kambi ya muda ya watani wao Yanga ambao walitaka kukimbilia huko.

MASHABIKI wa Simba waliopo Zanzibar hawawezi kuiona tena Yanga hivi karibuni labda kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka.

Hiyo inamaanisha kwamba hawatamuona kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko wala beki Mtogo Vincent Bossou.

Simba ipo Zanzibar kwa kambi ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara msimu ujao, lakini uwepo wao umefuta ratiba ya kambi ya muda ya watani wao Yanga ambao walitaka kukimbilia huko.

Yanga ilitaka kukimbilia Zanzibar mapema wiki hii lakini ratiba hiyo imeingia mwiba kufuatia Simba kuwa huko.

Kocha Mkuu wa Yanga Hans Pluijm alisema kwasasa anaendelea na mazoezi ya kikosi chake katika uwanja wa chuo cha Polisi jijini Dar es Salaam huku akisubiri wachezaji wake 11 walioko katika vikosi vya mataifa yao.

“Kuna timu nyingi kule sasa ni vigumu na sisi tukaenda huko, lakini tutaangalia hapo baadaye kama tutakuwa na nafasi ya kufanya kingine chochote kwa kujiandaa kama timu baada ya wachezaji wote kurudi,”alisema Pluijm.

“Najua kwamba ligi inapoanza kila timu tutakayokutana nayo itataka kuonyesha wana uwezo wa kutuzuia kwa kuwa wanacheza na bingwa mtetezi nalijua hilo na nimewaanda wachezaji wangu kupambana na hali hiyo, najua ubora wao wanachotakiwa kuhakikisha Yanga inashinda kulinda jina la klabu.

“Tangu nilipoanza kuifundisha Yanga kwenye msimu wa 2013/14 sikuwahi kupata nafasi ya kusajili wachezaji ninaowataka. Nilikuja Yanga na nilifundisha mzunguko wa pili wa Ligi ya 2013/14, kazi ambayo nilianza mwaka jana Januari na wakati huo usajili wa dirisha dogo ulikuwa umekamilika ukisimamiwa na aliyekuwa kocha wa Yanga, Ernest Brandts.

“Hata hivyo baada ya msimu huo kuisha niliachana na Yanga na kuhamia timu nyingine (Shoala FC ya nchini Saudi Arabia) na timu ilikabidhiwa kwa kocha Mbrazili, Marcio Maximo na alifundisha sehemu ya msimu uliopita kwa takribani michezo saba na dirisha la usajili lilivyofunguliwa, yeye ndiye aliyesajili kabla hajaachana na Yanga. Mimi nilipokabidhiwa kazi nilikuta ameshasajili hivyo kwa kiasi fulani ilininyima uhuru ingawa nilipambana na kufanikiwa kutwaa ubingwa.

“Mwaka huu naamini utakuwa mwaka wangu wa mafanikio zaidi, kikosi nimesajili mwenyewe kulingana na mahitaji ya falsafa yangu lakini nimesajili nikiangalia zaidi wachezaji wa kucheza kwa kiwango cha juu kwenye michuano ya kimataifa na Ligi Kuu.

“Nitahakikisha ninatwaa ubingwa mapema, pia nitahakikisha kuwa ninabaki kuwa na wachezaji wa kiwango cha juu zaidi Ligi Kuu kwa wao kutwaa mataji mbalimbali ya heshima kama mfungaji bora, mchezaji bora wa Ligi na mchezaji bora wa mwezi.”

Pluijm ana kikosi cha wachezaji 24 ambao ni Makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Benedict Tinocco, Mudathir Khamis na Deogratius Munishi ‘Dida’.

Mabeki; Juma Abdul, Oscar Joshua, Mwinyi Haji Mngwali, Pato Ngonyani, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Vincent na Bossou.

Viungo; Salum Telela, Andrey Coutinho, Haruna Niyonzima, Thabani Kamusoko, Said Juma, Godfrey Mwashiuya,

Deus Kaseke na Simon Msuva. Pia washambuliaji; Mateo Anthony Simon, Donald Ngoma, Malimi Busungu na Amisi Tambwe.