Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yatumia wimbo wa Ali Kiba kuikebehi Simba 

Muktasari:

  • Yanga imesimama mitaa ya Msimbazi kisha kuimba wimbo unaojulikana kama Mnyama ambao umepigwa na Kiba ukiwa ni maalumu kwa Simba huku wakicheza pamoja kwenye gari.

Yanga imefika Makao makuu ya mtani wake Simba, hapo kukaa kidogo lakini gumzo ni pale walipoamua kuwakebehi kwa kuimba wimbo wa klabu hiyo uliopigwa na msanii Ali Kiba.

Yanga imesimama mitaa ya Msimbazi kisha kuimba wimbo unaojulikana kama Mnyama ambao umepigwa na Kiba ukiwa ni maalumu kwa Simba huku wakicheza pamoja kwenye gari.

Mashabiki wa Yanga na viongozi wameimba wimbo huo huku wakionyesha vidole vitano juu wakiashiria mataji ambayo wameyabeba msimu huu.

Wakati wote Yanga wakiimba hivyo, mashabiki wa watani wao wamejikuta wakikaa kimya na kuwatazama tofauti na miaka ya nyuma ambapo walikuwa wakitoa makombe yao ya zamani na kujibu mapigo.

Kiungo wa Yanga Clatous Chama naye akaibuka na kutoa vuvuzela na kupulizia huku mashabiki wa Yanga wakishangilia kwa nguvu.

Huu ni msimu wa kwanza wa Chama akiwa na Yanga ambapo ameiongoza kutwaa makombe matano, Kombe la Ligi Kuu Bara, Ngao ya Jamii, Kombe la Muungano, Kombe la Toyota na Kombe la Shirikisho la CRDB.