Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yatumia saa tano paredi barabarani

SAA 5 Pict

Muktasari:

  • Kutoka uwanja wa ndege saa 7:20 mchana hadi kufika makao makuu ya timu hiyo imefika saa 11:52 jioni.

YANGA imetumia takribani saa tano kwenye paredi la ubingwa kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julisu Nyerere hadi kufika makao makuu ya timu hiyo, Jangwani.

Kutoka uwanja wa ndege saa 7:20 mchana hadi kufika makao makuu ya timu hiyo imefika saa 11:52 jioni.

Msafara huo umeongozwa na wachezaji wa timu hiyo wakiwangozwa na nahodha Bakari Mwamnyeto na viongozi wa timu hiyo akiwemo Rais Mhandisi Hersi Said.

Kuanzia paredi lilipoanzia ambalo lilijaza mashabiki waliowasindikiza wachezaji hadi walipofika Jangwani,

njiani watu walikuwa wengi wakiongozwa waendesha bodaboda zilizokuwa zimebeba mashabiki pia waliokuwa wanausindikiza msafara huo.

Aidha, kulikuwa na matukio kadhaa uwanjani ikiwemo basi lililowabeba wachezaji liliposimama mtaa wa Msimbazi na kuonyesha makombe kwa mashabiki wa Simba.

Matukio hayo yamekuwa mfululizo kwani Yanga wamekuwa wakiyafanya kila wanapobeba ubingwa kuanzia kipindi cha kocha Nassrredine Nabi, Miguel Gamondi na kocha wa sasa, Miloud Hamdi.