Yanga yatuma salamu

Wachezaji wa Yanga wakishangilia ushindi wao.
Muktasari:
Kwa ushindi Yanga inatakiwa ishiriki Kombe la Shirikisho Afrika lakini kwa kuwa ndiye bingwa wa ligi kuu na ana tiketi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nafasi ya Kombe la Shirikisho inakwenda Azam.
YANGA ina mechi ngumu na TP Mazembe kwenye Kombe la Shirikisho Afrika lakini jana Jumatano Uwanja wa Taifa ililaza Azam mabao 3-1 katika mechi ya fainali ya Kombe la FA na kubeba kombe hilo ikiwa ni salamu kwa wapinani wao wote wa Shirikisho.
Kwa ushindi Yanga inatakiwa ishiriki Kombe la Shirikisho Afrika lakini kwa kuwa ndiye bingwa wa ligi kuu na ana tiketi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nafasi ya Kombe la Shirikisho inakwenda Azam.
Jana Yanga walianza na bao dakika ya 9 lililofungwa kwa kichwa na Vincent Bosou baada ya kipa Aishi Manula kuupangua mpira.
Dakika ya 29 Farid Mussa alishindwa kuitumia vizuri pasi ya Mudathir Yahya baada ya shuti lake kutoka nje.
Kocha Azam, Dennis Kitambi alimtoa John Bocco na nafasi yake kuchukuliwa na Didier Kavumbagu ambaye aliipatia Azam bao dakika ya 48. Ni Yanga waliotangulia kupata bao la pili dakika moja kabla ya Azam lililofungwa na Amiss Tambwe kwa pasi ya Simon Msuva.
Kocha wa Yanga, Hans Pluijm aliwatoa Oscar Joshua na Haruna Niyonzima na kuwaingiza Haji Mwinyi na Mbuyu Twite na Bosou alitoka akaingia Nadir Haroub.
Bao la tatu la Yanga lilifungwa na Deus Kaseke kwa pasi ya Kamusoko.
Yanga: Deo Munishi, Juma Abdul, Oscar Joshua, Yondani, Niyonzima, Bosou, Msuva, Thaban Kamusoko, Tambwe, Ngoma na Kaseke.
Azam: Aishi Manula, Nyoni, Gidiel Michael, Moris, h Kheri, Mugiraneza, Ramadhan Singano, Muathir Yahaya, HMao, Farid Mussa na Bocco.
Nao, wachezaji wapya wa Yanga, Hassan Kessy na Juma Mahadhi jana walichangiwa fedha na mashabiki wa Yanga Uwanja wa Taifa. Mahadhi aliyesajiliwa Yanga kutoka Coastal na Kessy kutoka Simba nao walifika kuishuhudia timu yao mpya ikiiadhibu Azam ingawa hawakutaja fedha zilizochangwa ni kiasi gani.
Nayo timu ya vijana chini ya miaka 17 ya Serengeti Boys jana iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Malaysia na hivyo kushika nafasi ya tatu katika michuano maalum ya nchini India.