Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yatua Dar, Nabi atamba

KIKOSI cha Yanga kimewasili leo asubuhi saa 5:00 katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, Terminal 2 wakitokea mkoani Arusha katika mechi yao ya Ligi dhidi ya Polisi Tanzania.

Yanga walishinda 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania mchezo uliopigwa jana katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Baada ya kuwasili kocha mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amesema anajivunia kutoka na jumla ya pointi sita wakiwa ugenini.

Nabi amesema kupata pointi hizo ilitokana na morali ya ushindi ambayo wachezaji wake wamejiwekea wao wenyewe.

“Haikuwa rahisi kukaa nje ya Dar es Salaam kwa siku 10 lakini wachezaji wetu walikuwa na morali ya ushindi na kuhakikisha tunapata pointi sita zote,” amesema Nabi.

Nabi amesema anawasifu wachezaji wake kupambana katika mchezo wao dhidi ya Polisi Tanzania na kupata pointi tatu.

“Mechi ya kwanza tulicheza vizuri, hii hatukucheza vizuri inawezekana kutokana na uchovu lakini wachezaji walipambana,” amesema Nabi.

Yanga kwenye mechi zao za ugenini wameshinda zote mbili baada ya kuwafunga Coastal Union 2-0 na Polisi Tanzania 1-0.