Yanga yathibitisha Lamine kuondolewa kambini

Muktasari:

Wakati Yanga ikibakiza saa chache kushuka uwanjani kucheza dhidi ya wenyeji wao Namungo ya Lindi nahodha woa Mkuu beki Lamine Moro ameondolewa kambini na kurudishwa jijini Dar es Salaam.

Wakati Yanga ikibakiza saa chache kushuka uwanjani kucheza dhidi ya wenyeji wao Namungo ya Lindi nahodha woa Mkuu beki Lamine Moro ameondolewa kambini na kurudishwa jijini Dar es Salaam.

Yanga inashuka uwanja wa Majaliwa kucheza dhidi ya Namungo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaoanza majira ya saa 10:00 jioni.

Taarifa kutoka Yanga ni kwamba Lamine amekumbwa na kadhia hiyo akidaiwa kuwa na utovu wa nidhamu akitofautiana na kocha mkuu wa timu hiyo Nesreddine Nabi.

Yanga kupitia mtandao wao umethibitisha hilo kupitia Afisa Habari wa timu hiyo Hassan Bumbuli akisema beki huyo amekuwa akishindwa kufuata utaratibu wa wachezaji majeruhi.

"Kila mchezaji majeruhi kuna utaratibu anaufuata wa kutakiwa kuwepo mazoezini kuangalia kipi kinaendelea katika mazozei ya wengine lakini pia hata mtiririko wa matibabu yake timu ina madaktari ambao wanausimamia,"alisema Bumbuli.

Yanga sasa bada ya uamuzi huo ni wazi itabaki na mabeki watatu katika kikosi chao ambao ni nahodha msaidizi wa pili beki Bakari Mwamnyeto,Said Juma Makapu na Dickson Job wakati wakielekea katika mchezo dhidi ya Namungo.

Beki Abdallah Shaibu 'Ninja'hakusafiri na kikosi hicho kufuatia kuwa majeruhi ikielezwa alirejea kwao Zanzibar kupambana na matibabu hayo.