Yanga yathibisha Bangala ni mali ya Azam FC

Uongozi wa Klabu ya Yanga umethibitisha rasmi kuwa kiungo Mkongomani, Yannick Bangala atajiunga na matajiri wa Chamazi, Azam FC ambapo anaenda kuungana na Feisal Salum Abdallah maarufu kama Fei Toto.
Bangala ambaye anamudu kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani aliitumikia Yanga akitokea FAR Rabat ya Morocco na kufanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/2022.
Inatajwa kuwa Azam wametumia kiasi cha Sh100 milioni kumng’oa kiungo huyo kutoka vyunga vya Jangwani ambapo tangu awali alionekana kutokwepo kwenye mipango ya timu hiyo kuelekea msimu wa 2023/2024.