Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaoga minoti Zanzibar, yazawadiwa Sh100 milioni

Muktasari:

  • Yanga imefanikiwa kutwaa mataji matano msimu huu wa 2024/25 ikiwemo Ngao ya Jamii, Kombe la Toyota, Kombe la Muungano, Kombe la Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la CRDB.

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi ameizawadia klabu ya Yanga Sh100 millioni kwa kutambua ushindi na mafanikio makubwa ya klabu hiyo kwa msimu wa 2024/25.

Zawadi hiyo ameitoa leo Jumatatu 30, 2025 wakati alipokutana na viongozi na wachezaji wa timu hiyo Ikulu kwa ajili ya kukabidhiwa makombe matano waliyotwaa msimu huu.

Dk Mwinyi, ameishukuru klabiu hiyo kwa kuendelea kuitangaza Zanzibar ndani na nje ya nchi kupitia kampeni yale ya Visit Zanzibar na kucheza baadhi ya mechi zao visiwani humu.

Rais Mwinyi, amesema hatua ya klabu hiyo kucheza michezo yake Zanzibar imechangia kukuza uchumi na sekta ya utalii kwa kuongezeka idadi ya wageni na wananchi kunufaika na fursa mbalimbali.

"Mafanikio yaliyopatikana katika klabu yanu yanajenga heshima na historia muhimu katika tasnia michezo nchini," amesema Dk Mwinyi 

Hivyo, Dk Mwinyi ameahidi kuwa serikali itaimarisha viwanja vya michezo kwa lengo la kuwezesha michuano mingi kufanyika Visiwani hapa.

Naye, Rais wa Yanga, Hersi Said Ali amemkabidhi Dk Mwinyi medali maalumu na jezi ya ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League).

Pia Hersi ametoa shukrani na pongezi kwa Dk Mwinyi juhudi kubwa anazozifanya za kuimarisha miundombinu ya michezo na timu hiyo imeahidi kucheza mechi zake hapa.