Yanga yamshusha Mayele rasmi

Muktasari:

Yanga imefanya kweli ikimshusha nchini mshambuliaji Fiston Mayele tayari kwa kuja kumsainisha mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo.

Yanga imefanya kweli ikimshusha nchini mshambuliaji Fiston Mayele tayari kwa kuja kumsainisha mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo.

Mayele ametua nchini leo mchana akitokea kwao DR Congo akija na meneja wake Nestor Mutuale akipokea na mmoja wa vigogo wa Yanga Godson Karigo.

Mayele anakuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni kutua nchini katika dirisha kubwa la usajili huku nyuma yake akitarajiwa kuja beki Shaban Djuma ambaye Yanga tayari ilishamsainisha mapema mkataba wa miaka miwili.

Msimu uliopita Mayele alikuwa ameitumikia AS Vita akibuka mshambuliaji wa pili kinara wa ufungaji katika ligi ya nchini DR Congo akipachika mabao 13 akizidiwa bao moja pekee na Jean Baleke wa TP Mazembe aliyepachika mabao 14.

Hatua ya ujio wa Mayele ni kwamba Yanga imeanza kufanyia kazi changamoto za kupachika mabao ambapo msimu uliopita ambapo msimu uliomalizika hakuna mshambuliaji aliyefanikiwa kufunga hata mabao 9 katika ligi.

Mfungaji bora ndani ya Yanga katika msimu uliomalizika ni Yacouba Sogne aliyefunga mabao 8 akifutiwa na kiungo Deuse Kaseke aliyefunga mabao 6.