Yanga yaja kivingine ikimkosa Djuma

KOCHA mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amepangua kikosi chake kimtindo kwa kufanya badiliko moja kwenye kikosi cha kwanza wakiikabili Mbeya City leo usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Nabi amempumzisha Yassin Mustapha huku akimkosa Djuma Shaban anayetumikia adhabu ya mechi tatu baada ya kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Polis Tanzania.
Wakati wachezaji hao wakikosekana, kiungo Feisal Salum ambaye alikuwa nje akisumbuliwa na majeraha amerejea na kuanzia benchi.
Kikosi kamili cha Yanga ni Aboutwalib Mshery, David Bryson, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Zawadi Mauya, Yannick Bangala, Khalid Aucho, Jesus Moloko, Farid Mussa, Saido Ntibazonkiza na Fiston Mayele.
Wachezaji wa akiba ni Erick Johora, Paul Godfrey, Ibrahim Bacca, Dickson Ambundo, Salum Aboubakary 'Sure Boy', Nico Ushindi, Deus Kaseke, Feisal Salum 'Fei Toto' na Heritier Makambo.
Mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara kwa timu hizi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ulipigwa Septemba 13, 2020, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na beki wao wa zamani Lamine Moro.
Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 35, wakati Mbeya City inashika nafasi ya nne na pointi 22, baada ya kila timu kucheza michezo 13.