Yanga yaifuata Dodoma Jiji kibabe

Friday May 13 2022
Yanga PIC
By Thomas Ng'itu

KLABU ya Yanga imeondoka leo kwenda jijini Dodoma kwa ajili ya mchezo wao ujao dhidi ya Dodoma Jiji utakaochezwa Jumapili ya Mei 15,  saa 10:00 alasiri katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mwanaspoti Online ambalo lilikuwa katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 lilishuhudia kikosi cha Yanga kikiondoka huku mastaa wake  wakiwa na nyuso za furaha.

Kocha Nasreddine Nabi wa Yanga katika kuhakikisha hataki masihara ameondoka na mastaa wake wote kasoro Chico Ushindi, Yacouba Sogne na David Bryson ambao wote wana majeraha huku Paul Godfrey na yeye akikosekana kwenye msafara huo.

Kwenye msafara huo yupo kiungo Salum Abubakari ‘Sure Boy’ ambaye awali kulikuwa na tetesi za kutosafiri kutokana na kuugua Malaria ghafla.

Yanga inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kuongeza gepu la pointi dhidi ya Simba ikiwa ni sehemu ya mbio za Ubingwa msimu huu.

Timu hiyo inashika nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 57 huku Simba ikiwa n pointi 49.

Advertisement

Mastaa walioondoka ni Djigui Diara, Abuutwalib Mshery, Eric Johora, Kibwana Shomari, Djuma Shaban, Yassin Mustapha, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Denis Nkane na Yanick Bangala.

Wengine ni Salum Abubakari, Feisal Salum, Bacca, Khalid Aucho, Zawadi Mauya,Jesus Moloko, Farid Mussa, Dickson Ambundo , Crispin Ngushi na Deus Kaseke, Saido Ntibazonkiza, Feisal Salum na Heritier Makambo.

Advertisement