Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaanza Kizungu, yatumia teknolojia ya kisasa kwa mastaa

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • YANGA juzi ilianza mikwara yake kama kawaida baada ya kurudi kambini huku wachezaji wakifika na kuanza kupimwa utimamu wa mwili na vifaa maalumu vya kisasa kama inavyokuwa kwenye klabu zilizoendelea za Ulaya.

YANGA juzi ilianza mikwara yake kama kawaida baada ya kurudi kambini huku wachezaji wakifika na kuanza kupimwa utimamu wa mwili na vifaa maalumu vya kisasa kama inavyokuwa kwenye klabu zilizoendelea za Ulaya.

Yanga ilianza mazoezi hayo ikiwa inajiandaa na kwa ajili ya mechi zijazo za ligi, Kombe la Azam na Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi, huku wakionekana kupania kuendelea na kasi yao.

Kocha wa timu hiyo, Mrundi, Cedric Kaze ndiye aliyekuwa akisimamia mazoezini hayo lakini akiwa na faili lote kutoka kwa kocha mkuu wa timu hiyo, Nassredine Nabi ambaye atarejea muda wowote akitokea likizo kwao Tunisia.

Baada ya kutua Avic Town, Kigamboni iliko kambi ya timu hiyo, wachezaji wote wa Yanga kabla ya kufanya kitu chochote mazoezini walianza kwa kupimwa utimamu wa mwili chini ya Kocha wa Viungo, Helmy Gueldich, ili kuhakikisha wamefanyia kazi kile walichoelekezwa na Nabi kabla ya kuondoka, huu ukiwa ni mfumo ambao unatumiwa na timu nyingi kubwa barani Ulaya.

Wakati ligi inasimama kupisha Kombe la Mapinduzi, Yanga iliwapa mapumziko mastaa wake kadhaa ili wakapate nafasi ya kuonana na familia zao lakini haikuwaacha hivihivi bali iliwapa programu maalumu za mazoezi na kuwataka wazifanye kwa ukamilifu wakiwa makwao na hivyo walivyorejea benchi la ufundi la timu hiyo lilianza kuangalia na kupima kila mchezaji kama alifuata programu kwa usahihi.

Hata hivyo, mtaalamu huyo alionekana kukubaliana na kila mchezaji kwani wote walionekana kufanyia kazi mazoezini waliyopewa kwa ufasaha ingawa na yeye ataanza programu nyingine ngumu kuanzia leo Jumamosi.

Katika mazoezi ya siku mbili nyuma kuna baadhi ya mastaa wa timu hiyo walikuwa hawajawasili kikosini hapo lakini sasa wapo kamili maandalizi ni ya mechi ya ligi dhidi ya Ihefu itakayopigwa Januari 16, katika Uwanja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kipa Djigui Diarra na kiungo Mganda Khalid Aucho ni miongoni mwa wachezaji ambao hawakuwepo lakini leo wanatarajiwa kujiunga na wenzao na watapimwa pia kabla ya mazoezi.

Aucho alionekana mara kwa mara kwenye peji yake ya Instagram akifanya mazoezini ya kukimbia na na kunyoosha misuli ikiwa ndiyo programu aliyopewa na mabosi wake.

Yanga inajiandaa kulipa kisasi kwa Ihefu ikiwa ndio timu pekee iliyoifunga msimu huu baada ya kulala mabao 2-1 kwenye mchezo wa ligi na kuvunja utemi wa Wana Jangwani hao kwa kucheza michezo 49 mfululizo bila kupoteza.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha Kaze amesema wanaendelea kukiandaa kikosi kwa ajili ya mechi zijazo ikiwemo ya Ihefu wanayoamini itakuwa ngumu kwao.

“Wachezaji wanaendelea kuwasili kikosini na kuendelea na programu za mazoezi, kwa sasa jicho letu zaidi ni kwa mechi zijazo ikiwemo ya kwanza na Ihefu, tulipoteza mechi dhidi yao lakini hatutaki kufanya makosa tena hivyo tunaandaa timu ili kushinda,” alisema Kaze.

Yanga hadi sasa ndiyo inaongoza Ligi Kuu ikiwa na alama 50 kileleni baada ya kucheza mechi 19, kushinda 16 sare mbili na kupoteza mchezo mmoja.