Prime
Yanga yaangukia pua rufaa ya Aucho TFF

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imejadili maombi ya marejeo ya klabu ya Yanga kuhusu adhabu ya kufungiwa michezo mitatu 3 na kutozwa faini ya Sh500,000 iliyotolewa kwa mchezaji Khalidi Aucho kupitia kikao cha kamati hiyo Novemba 14, 2023.
Aucho alikumbana na adhabu hiyo kutokana na kosa la kumpiga kiwiko nahodha wa Coastal Union, Ibrahim Ajibu katika mchezo namba 71 uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Hata hivyo baada ya kupitia maelekezo ya klabu ya Yanga na kanuni za Ligi kamati imejiridhisha kwa mara nyingine kuwa adhabu iliyotolewa kwa mchezaji huyo ni sahaihi hivyo anapaswa kuendelea kuitumikia huku ikimtaka kuzingatia michezo ya kiungwana wakati wote.
Yanga ilikata rufaa hiyo siku moja baada ya Kamati ya Bodi ya Ligi kutangaza kumfungia kiungo huyo kwa mechi tatu na faini ya Sh500,000 kwa kosa la utovu wa nidhamu.