Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga watua kibabe kwa Mkapa

KLABU ya Yanga imetua kibabe katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10:15 jioni huku wakiingia mlango tofauti na uliyozoeleka.

Yanga kama kawaida waliingia na gari lao kubwa na kupita mlango karibu na uwanja wa Uhuru na kuachana na mlango mkubwa unaotumika kuingia kwa magari makubwa.

Walipofika uwanjani mashabiki wa klabu hiyo waliisapoti timu yao kwa kulifata gari nyuma mpaka lilipopaki.

Pia timu hiyo haikupitia katika mlangk mlangk uliozoeleka timu kuingia badala yake walipita katika mlango wa kuingilia upande wa mikutano ya Waandishi wa Habari.

Yanga imewasili ikiwa ni dakika chache baada ya Uongozi wa Yanga kutoa taarifa ya kupeleka timu muda ambao mchezo ulipangwa kuchezwa saa 11:00 na sio saa 1:00 usiku.