Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga waitangulia Simba Airport

KIKOSI cha Yanga kimetua jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo Februari 14 kutokea jijini Mbeya baada ya kumaliza mchezo wao wa jana dhidi ya Mbeya City na kutoka sare ya bao 1-1.

Yanga wamerudi kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Kagera Sugar Februari 17 utakaopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Bao pekee la Yanga jana lilifungwa na Deus Kaseke dakika ya 85 alipomalizia mpira uliowashinda mabeki kuutoa eneo la hatari huku Mbeya City wakisawazisha kwa penalti baada ya Yasin Mustapha kuunawa mpira ndani ya boksi.

Wakati Yanga wakitua asubuhi leo watani wao Simba SC wataingia saa 7 mchana wakitokea Ethiopia walipolala baada ya kuanza safari DR Congo walipotoka kuiua AS Vita bao 1-0.

Simba inashikiri hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika na mchezo wa kwanza walianzia ugenini na Chris Mugalu kuifunga AS Vita kwa mkwaju wa penalti.

Simba jana walikataza mashabiki wao kuwapokea hadi watapomaliza lengo lao la kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa Afrika.

Simba mchezo ujao watacheza na Biashara United uwanja wa Karume mjini Musoma Februari 18 kabla ya kuvaana na Al Ahly Februari 23 jijini Dar.