Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga sasa ni straika Mkongo

YANGA iko katika mazungumzo na mastraika wawili hatari lakini kati ya hao mmoja wa haraka ambaye anatakiwa na kocha wao Nesreddine Nabi ni Fiston Mayele wa AS Vita ya DR Congo.

Nabi anataka Mayele awe chaguo namba moja katika mipango ya msimu ujao na akiwapiga mkwara mabosi wake kwamba hataki kumkosa huyo jamaa ingawa kimahesabu ni miongoni mwa wachezaji ghali wa Vita.

Mayele ndio mfungaji wa pili katika vinara wa mabao msimu uliomalizika pale DR Congo akiwa na mabao 13 akizidiwa bao moja tu ya Jean Baleke wa mabingwa wa nchi hiyo TP Mazembe mwenye mabao 14 akiwa mfungaji bora.

Taarifa za Mayele tayari zipo mezani kwa Ghalib Said, Bilionea na mmoja wa wadhamini wa Yanga kupitia GSM, ambaye anachofanya sasa ni mkakati wa kumshusha nchini haraka mshambuliaji huyo anayelijua goli. Mayele pale AS Vita ndiye aliyeziba nafasi ya Jean Makusu Mundele baada ya kuondoka ingawa

Mwanaspoti kuwa wawili hao wote Nabi anawatamani awapate kwa mpigo. Nabi katika kumuinda Mayele tayari ameshazungumza naye na Mwanaspoti linafahamu mshambuliaji huyo anasubiri simu ya mwisho ya mabosi wa Yanga. Mayele mara ya mwisho kukanyaga Dar alitua na DR Congo ya wachezaji wa ndani kisha akamfunga kipa Juma Kaseja bao moja.