Yanga Princess yakoga pesa Taifa

DAKIKA kadhaa baada ya kuwapa mashabiki wa Yanga raha ya ushindi kwa kuibamiza Ilala Queens mabao 4-0 kwenye mchezo wa kirafiki wa kuhitimisha Wiki ya Mwananchi, wachezaji wa Yanga Princess wamekoga pesa kutoka kwa mashabiki.

Baada ya mechi iliyopigwa Uwanja wa Mkapa wachezaji wa Yanga Princess walienda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo huku wakishangiliwa.

Zilipita dakika kadhaa kabla ya mabinti hao kurejea tena uwanjani na kuanza kuwasalimia mashabiki ambao waliwapokea kwa shangwe.

Mbali ya shagwe mashabiki hao walianza kuwarushia pesa ambazo wachezaji hao walizikusanya vyema na kuzihifadhi kwenye jezi zao na wengine wakawa wanaziingiza kwenye soksi.