Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga noma, yatawala kila kona

Noma Pict
Noma Pict

Muktasari:

  • Hizi zote ni shamra shamra za kuchangamsha siku ya Wananchi, huku mechi hiyo ikiwaacha mashabiki na vicheko maana licha ya ushindani mkubwa uliokuwepo vimbwanga huku navyo havikukosekana.

YANGA imeendelea kufanya vizuri kila kona baada ya kikosi hicho cha Maveterani kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Wasanii, katika mchezo wa utangulizi kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi.

Hizi zote ni shamra shamra za kuchangamsha siku ya Wananchi, huku mechi hiyo ikiwaacha mashabiki na vicheko maana licha ya ushindani mkubwa uliokuwepo vimbwanga huku navyo havikukosekana.

Mechi hiyo iliyochezwa ndani ya dakika 90, bao la kwanza lilifungwa na msanii Fobi lakini baadae Yanga waliamka na kuanza kuuwasha moto mpaka kocha wa timu ya Wasanii kuingia uwanjani baada ya mchezaji wake kufanyiwa madhambi na kushindwa kufunga bao.

Wakati wa mchezo huo ukiendelea kipindi cha kwanza aliingia Mtumbuizaji mashuhuri Christian Bella na kufanya mashabiki wa Yanga kupata burudani mara mbili.

Viongozi walioshiriki katika mechi upande wa Yanga ni pamoja na Makamu wa Rais wa kikosi hicho Arafat Haji ndiye aliyekuwa nahodha wa kikosi hicho cha maveterani na maofisa wa Yanga dhidi ya masupastaa waliongozwa na kina Yusuf Mlela na wengineo.