Yanga ndio basi tena Kagame Cup… yapigwa 3 na Express kwa Mkapa

KIPA wa Yanga, Ramadhan Kabwili amekuwa na gundu katika michuano ya Kombe la Kagame, baada ya mechi alizocheza kuambulia maumivu.
Mechi ya kwanza alipata kadi nyekundu dhidi ya Malawi na mchezo wake wa pili dhidi ya Express amepigwa mabao 3-1.
Kitendo cha Yanga, kufungwa mchezo wa leo kimewaondoa kwenye michuano hiyo, imetoka sare mbili, imefungwa mmoja na wanamiliki mabao mawili tu.
Kipindi cha pili Yanga ilikosa mipango kabisa ya kusawazisha mabao 2-0 waliofungwa kipindi cha kwanza, badala yake wakaongezwa bao lingine.
Bao la tatu la Express lilifungwa na Erick Kenzo, liliwaongezea nguvu ya kuishambulia zaidi ya Yanga na kuwafanya mabeki kufanya makosa Ninja alipewa kadi ya njano, kutokana na kucheza rafu.
Vijana wa Yanga B waibua shangwe kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kupata nafasi ya kucheza wakichukua nafasi ya Waziri, Ukonde aliingia Adam Kiondo na Said Kwangala.
Kuingia kwao kuliwapa bao Yanga kupitia kwa Poul Godfrey 'Boxer' aliyepiga shuti nje ya 18 lililomshinda kipa na kutinga nyavuni.