Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga na KMC kupigwa Machi 19, Simba yapewa kiporo

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko ya mchezo namba 144, kati ya Yanga na KMC zote kutoka Jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa leo Machi 10 na TPLB imeeleza mchezo huo utachezwa Machi 19 badala ya Machi 16 kama ilivyopangwa hapo awali huku sababu kubwa ikiwa ni kupisha marekebisho ya miundombinu ya Uwanja wa Benjamin Mkapa yaliyopangwa kufanyika kuanzia Machi 15-18, 2022.

Katika hatua nyingine mchezo namba 142, wa Ligi Kuu Bara kati ya Polisi Tanzania dhidi ya Simba uliopagwa kufanyika Machi 27, kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi umeahirishwa ili kupisha michezo ya kirafiki ya Taifa ya Tanzania ilipo kwenye kalenda ya FIFA.

Bodi hiyo imezitakia maandalizi mema ya michezo inayofuata klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Bara kwa msimu huu wa 2021/22.