Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga ile ile, yarudi kileleni

Straika wa Yanga, Donald Ngoma (jezi namba 11) akiwa chini ya ulinzi mkali wa wachezaji wa Ndanda FC wakati wa mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa jana Jumapili katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda bao 1-0. PICHA | OMAR FUNGO

Muktasari:

Mabingwa watetezi hao walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda ya Mtwara

YANGA jana Jumapili ilirejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara, lakini gumzo likiwa ni ugonjwa unaoisumbua timu hiyo katika suala zima la upigaji penalti.

Mabingwa watetezi hao walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda ya Mtwara, huku kinara wa mabao Amissi Tambwe akipoteza penalti ambayo ingewapa uongozi wa mapema kwenye kipindi cha pili cha mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Tambwe alipoteza penalti hiyo katika dakika ya 46 baada ya Paul Ngalema kumuangusha Simon Msuva, lakini mkwaju wake uligonga besela na kurudi uwanjani na kupiga shuti jingine lililookolewa na kipa wa Ndanda, Jeremia Kisubi.

Yanga imekuwa na tatizo la upigaji wa penalti ikishuhudiwa mara kadhaa nyota wake wakiikosesha timu hiyo ushindi na hata kupoteza michezo yao katika hatua hiyo kama ilivyokuwa kwenye nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi iliyochezwa hivi karibuni visiwani Zanzibar.

Hata hivyo baada ya Tambwe kupoteza penalti hiyo muhimu, dakika chache baadaye Yanga ilipata tena penalti nyingine katika dakika ya 57 baada ya Deus Kaseke kuangushwa langoni na mwamuzi Mathew Akrama kuamuru pigo hilo.

Safari hii beki Kelvin Yondani hakufanya makosa alikwamisha mpira huo kimiani baada ya kumpora mpira Simon Msuva aliyekuwa akitaka kuipiga, ambapo mashabiki wa Yanga walimkataa na kumtaka kipa Deo Munishi ‘Dida’ akapige, ila Yondani akatumia utemi na kwenda kuifunga kuiandikia Yanga bao pekee.

Bao hilo lililowapa ushindi Yanga limeifanya timu hiyo kuvuna pointi tatu na kufikisha jumla ya pointi 36 ikilingana na Azam, iliyokuwa ikiongoza msimamo ambayo sasa inashuka hadi nafasi ya pili kwa kuzidiwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa na Yanga, japo zote zimecheza mechi 14 kila moja.

Katika pambano hilo, Yanga itabidi ijilaumu kwa kushindwa kuibuka na ushindi mnono mbele ya ‘Wana Kuchele’ ambao walionyesha upinzani mkubwa katika kipindi cha kwanza kuwabana nyota wa Yanga wasifurukute huku kipa wao, Kisubi akiokoa michomo kadhaa hatari langoni mwake.

Uchezaji wa kibabe uliiponza Ndanda na kujikuta wakisababisha penalti hizo mbili, ambapo ya Tambwe iliota mbawa kabla ya Yondani kukwamisha na kuipa Yanga ushindi huo muhimu.

Donald Ngoma, Tambwe na Simon Msuva walikosa mabao kadhaa ya wazi, huku Ndanda kupitia kwa Atupele Green ilikaribia kuiumbua Yanga kama sio papara ya wachezaji wake mbele ya langop la vijana wa Hans Pluijm.

Katika pambano hilo timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji na pia kupata pigo kwa kila upande kumpoteza mchezaji kwa sababu ya kuumia, Yanga ikipata pigo kwa Deus Kaseke katika kipindi cha pili na Ndanda katika klipindi cha kwanza baada ya Jackson Nkwera kuumia na kumpisha Omega Seme.

Kwa kipigo hicho Ndanda inayonolewa na Hamimu Mawazo imesaliwa na pointi zake 9 na kukaa nafasi ya tatu kutoka mkiani.

Yanga: Deo Munishi, Juma Abdul, Oscar Joshua, Vincent Bossou, Kelvin Yondani, salum Telela, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Amissi Tambwe/Malimi Busungu na Deus Kaseke/ Issofou Boubacar.

Ndanda: Jeremia Kisubi, Aziz Sibo, Paul Ngalema, Cassian Ponera, Salvatory Ntebe, Jackson Nkwera/ Omega Seme, William Lucian, Hemed Khoja, Atupele Green, Kiggy Makassy na Braison Raphael/Masoud Ally.