Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga hii! yoyote anakupiga, wadau wasema itakuwa balaa

KOCHA mkuu wa Yanga, Cedric Kaze mpaka sasa bado hajapata safu kamili ya ushambuliaji katika kikosi chake licha ya kwamba timu yake imepata matokeo katika mechi zake zote mbili alizoziongoza akiwa katika benchi la kikosi hiko.

 

Kaze aliyejiunga na timu hiyo Oktoba 16 kwa kuitumikia timu hiyo miaka miwili, katika mechi zake zote mbili za mwanzo ameibuka na ushindi licha ya kwamba hajawa na pacha kamili katika eneo la ushambuliaji.

 

Katika mchezo wao dhidi ya Polisi Tanzania walioshinda 1-0, Kaze kwenye eneo la ushambuliaji aliwaanzisha Yacouba Sogne na Haruna Niyonzima huku goli la ushindi likifungwa na Tonombe Mukoko.

 

Mchezo wake wa pili dhidi ya KMC, Kaze katika eneo la ushambuliaji aliwapanga Michael Sarpong na Waziri Junior na kupata ushindi wa mbao 2-1 yaliyofungwa na Tuisila Kisinda na Waziri Junior.

 

Kwa upande wa Kaze alisema lengo lake yeye ni kuhakikisha kila mchezaji anakuwa sehemu ya timu kwa kupata nafasi ya kucheza.

 

"Kila mchezaji nitampa nafasi ya kucheza na kuona uwezo wake lakini pia kujiona sehemu ya timu, lengo ni kupata matokeo."

 

Upande wa wadau walionekana kubariki hali ya kocha huyo kufanya mabadiliko katika eneo la ushambuliaji ili kuweza kupata kombinesheni nzuri kama ambavyo alivyoweza kuipata katika maeneo mengine.

 

Aliyewahi kuwa mchezaji wa Simba na Yanga kwa nyakati tofauti, Zamoyoni Mogela alisema mwalimu bado anatafuta pacha sahihina ni jambo zuri kwake ili kuwa na watu sahihi katika kikosi cha kwanza.

 

"Siwezi kusema yupi ni bora lakini baada ya mechi tano wachezaji bora watajitenga , kwenye mpira hakuna upendeleo kama ambavyo watu wanasema lakini uwanjani ukifanya vizuri basi utapata nafasi."

 

"Baada ya mechi tani atapata timu ya ushindi lakini kocha aachwe huru afanye kazi, apewe nmuda na mashabiki wanatakiwa watambue hilo sio timu ikipoteza basi waanze mambo yao."

 

Kwa upande wa Ally Mayai ambaye ni mchezaji wa zamani katika timu hiyo na sasa ni mchambuzi wa soka nchini, alisema kocha bado hajapata hata kombinesheni sahihi katika kikosi chake lakini akiipata Yanga itakuwa vizuri zaidi ya sasa.

 

"Kocha anataka timu iwe inacheza mna ndio maana bado anataka kutengeneza kombinesheni nzuri,  anatumia mifumo tofauti tofauti ili kutengeneza timu kwahiyo siwezi kusema atachukua mechi ngapi, lakini atakapopata kombinesheni timu itakuwa vizuri zaidi ya sasa."

 

Kaze katika mchezo wao dhidi ya Polisi Tanzania, aliwaanzisha Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Yassin Mustafa, Bakari Mwamnyeto, Lamine Moro, Tonombe Mukoko, Tuisila Kisinda, Feisal Salum, Yacouba Sogne, Haruna Niyonzima na Farid Mussa.

 

Kwenye mchezo dhidi ya KMC aliwaanzisha Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Yassin Mustafa, Bakari Mwamnyeto, Lamine Moro, Tonombe Mukoko, Tuisila Kisinda, Feisal Salum, Michael Sarpong, Waziri Junior na Deus Kaseke.