Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga helua helua

Wachezaji wa yanga wakiwa nchini Misri jana kabla ya mechi kuanza.

Muktasari:

Yanga ambayo sasa imeangukia katika Kombe la Shirikisho Afrika ambapo leo Alhamisi itajua itakutana na nani, ilifungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Borg El Arab, mjini Alexandria.

MABINGWA wa Tanzania, Yanga imeaga michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa bao la jioni na wenyeji wao Al Ahly, lakini ikiacha gumzo Misiri kwa soka lake la kiwango cha hali ya juu kilichowaduwaza wenyeji wao.

Yanga ambayo sasa imeangukia katika Kombe la Shirikisho Afrika ambapo leo Alhamisi itajua itakutana na nani, ilifungwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Borg El Arab, mjini Alexandria.

Kipigo hicho kiliifanya iage kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya sare ya 1-1 nyumbani.

Bao la dakika za nyongeza lililofungwa na Abdallah Said lilizima ndoto za Yanga pengine kuingia muda wa nyongeza na hata hatua ya penalti kama ilivyofanya mwaka 2014 mbele ya mabingwa hao wa kihistoria wa Afrika.

Wenyeji walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 53 kupitia kwa Hossam Ghaly akiunganisha kwa kichwa krosi ya Ahmed Fathi mpira ambao ulimchanganya kipa Deo Munishi na kujaa wavuni.

Hata hivyo Donald Ngoma aliisawazishia Yanga bao dakika ya 67 pia kwa kichwa akimalizia krosi ya Juma Abdul, kisha Yanga kusakata soka la hali ya juu lililofanya mashabiki wa Al Ahly kushindwa kuamini kama wanaocheza nao ni Yanga.

Hilo lilikuwa bao la kwanza kwa Yanga ndani ya dakika 90 katika ardhi ya Waarabu tangu mwaka 1992 walipotoka sare ya bao 1-1 na Ismailia ikiwa na maana ni miaka 24 iliyopita.

Hata hivyo wakati mashabiki wengi wakiamini mechi imeisha kwa sare, sekunde chache kabla ya dakika tano za majeruhi kumalizika, Abdallah aliyetokea benchi aliivusha Al Ahly kwa kufunga bao la kichwa akimalizia krosi ya Walid Soliman.

Wachezaji wa Yanga hawakuamini wakati kipyenga cha mwisho cha mwamuzi, Mahamadou Keita kutoka Mali kilipolizwa kuashiria kumalizika kwa pambano hilo.

Licha ya kufungwa Yanga ilicheza kwa uelewano mkubwa ikiwabana wenyeji wao huku Thabani Kamusoko na Haruna Niyonzima wakithibiti eneo la kati.

Sasa Yanga inasubiri kujua itacheza na nani katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, huku kukiwa na hatari ya kukutana na timu nyingine ya Waarabu.

Timu zilizopenya hatua hiyo ni Esperance-Tunisia, Stade Gabesien-Tunisia, FUS Rabat-Morocco, Sagrada Esperanca-Angola, Misr El Makasa-Misri, Medeama-Ghana, na CF Mounana-Gabon zilizopenya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho.

Klabu nyingine ni zile zilizong’oka Ligi ya Mabingwa ikiwamo waliokuwa watetezi, TP Mazembe-DR Congo iliyovuliwa taji jana na Wydad Casablanca ya Morocco. Mbali na Mazembe pia zipo El Merreikh-Sudan, Al Ahli Tripoli-Libya, MO Bejaia-Algeria, Stade Malien-Mali, Mamelodi Sundonws na Etoile du Sahel.

Yanga: Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Vincent Bossou, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Thaban Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Donald Ngoma, Amissi Tambwe/Malimi Busungu na Deus Kaseke/Kelvin Yondani.