Yacouba, Saido ndani, Mtibwa wacheeeka!

SURA mbili mpya zinaweza kuingia kwenye kikosi cha Yanga leo kitakachoivaa Mtibwa katika Uwanja wa Mkapa huku uongozi ukisisitiza kwamba lazima kieleweke.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Yacouba Sogne na Saido Ntibazonkiza japo huenda wasicheze dakika zote tisini lakini leo watakuwepo kwenye kikosi kwani jana walichachafya mazoezini wakitokea majeruhi.

Kwa mujibu wa mazoezi ya jana, Kocha Cedric Kaze alikuwa mbogo kwelikweli huku akiwasisitiza wachezaji kutorudia makosa.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Hata hivyo kuna uhakika mkubwa kwamba Kaze leo anaweza kuwa na mabadiliko katika kikosi chake cha kwanza na yanaweza kugusa idara zote tatu muhimu.

Katika mazoezi ya jana ambayo yalitumia masaa mawili yalinogeshwa na ufundi na umakini jumla ya wachezaji 25 wa timu hiyo akiwemo Saido na Yacouba.

Katika mazoezi hayo Kaze alikuwa akionyesha dalili ya kuwajaribu kiungo Said Juma kucheza kati akitaka kuona nguvu kubwa inaongezeka katika kuimarisha safu ya ulinzi huku pia kipa Farouk Shikhalo akianza na Metacha Mnata akirudi benchi.

Muda mwingi Kaze alionekana kuelekeza akili yake katika kusuka safu ya ulinzi sambamba na safu ya ushambuliaji akitaka kuona wanapata matokeo na kulinda ushindi wao.

Pasua kichwa kwa Kaze ilikuwa katika safu ya ushambuliaji ambapo alikuwa akimjaribu Yacouba ingawa baadaye akambadilisha na kumpa nafasi Farid Mussa.

Pia akili nyingine ya Kaze ilikuwa kuwapima Ditram Nchimbi na Carlinhos.

Mbali na hao pia Kaze alikuwa akimjaribu Saido akipishana na Michael Sarpong huku pia Waziri Junior naye akipata nafasi.

Ushindani katika mazoezi hayo ulikuwa wa kiwango kinachoshtua ambapo wachezaji walionekana kuwa makini wakipambana mithili ya wapo katika mechi kamili.

Mmoja wa viongozi wa Yanga aliyekuwepo mazoezini hapo alidai kuwa wachezaji wameahidi kupambana kiume kuleta mabadiliko na kuondoa sintofahamu iliyopo.