Wydad yanusa ubingwa AFL

Wydad Casablanca imenusa ubingwa wa African Football League ba,ada ya kuichapa Mamelodi Sundowns mabao 2-1 jana katika Uwanja wa Mohamed V nchini Morocco.
Mabao ya Wydad yamefungwa na Rivaldo Coetzee dakika ya 41 na kipindi cha pili lilifungawa na Anas Serrhat huku Mamelodi wakipata bao dakika ya 74 na Abdelmounaim Boutouil.
Mechi ya marudiano itaamua bingwa wa kwanza AFL Novemba 12 katika dimba la Lucas Masterpieces Moripe, Afrika Kusini.
Mamelodi inakisasi na Wydad baada ya kutolewa kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita ambapo Wydad Casablanca ya Morocco iliyomuondosha katika mashindano hayo kwa mabao ya ugenini.