Wenger amtega Ozil

Muktasari:

Kiungo huyo wa Ujerumani amekuwa na wakati mgumu katika kikosi cha Arsenal msimu huu

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amedai ana uhakika kiungo wake Mesu Ozil ana nia ya kuendelea kukipiga klabuni hapo licha ya mkataba wake kutarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Inadaiwa kuwa klabu kubwa hazijaonyesha nia ya kumtaka staa huyo wa kimataifa wa Ujerumani licha ya uvumi kudai kwamba Manchester United imekuwa ikimfuatilia na Wenger sasa anaamini kuwa Ozil anataka kubakia Emirates.

Katika hatua nyingine Arsenal imeingia vitani na Chelsea na Manchester City katika kuisaka saini ya chipukizi wa Barcelona, Abel Ruiz, 17 ambaye ana kipengele kinachomruhusu aondoke klabuni hapo kwa dau la pauni 3 milioni tu.

Luiz amekuwa akitesa katika kikosi cha Hispania chini ya umri wa miaka 17 katika mashindano ya kombe la dunia inayoendelea nchini India na ameisaidia timu hiyo kutinga katika hatua ya 16 bora ambapo wanatazamiwa kucheza na Ufaransa.