Waziri Bashungwa afungua rasmi Canaf 2021

Waziri Bashungwa afungua rasmi Canaf 2021

WAZIRI wa Sanaa utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa ambaye ndiye mgeni rasmi wa ufunguzi wa mashindano ya barani Afrika ya soka kwa watu wenye ulemavu ameyafungua rasmi mashindano hayo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Waziri Bashungwa amewataka Watanzania kujivunia kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya sita hapa barani Afrika ya soka kwa watu wenye ulemavu kwani sio jambo dogo.

"Mashindano haya yatatumika kama Chombo cha kuongeza umoja baina ya Waafrika wote bila kusahau upendo hivyo mashindano haya ni muhimu sana kwetu"

"Ni wajibu wetu kama nchi kushiriki katika michezo inayohusisha watu walemavu huku tukiwapa fursa ya kushiriki katika michezo mbalimbali watu wenye ulemavu jambo ambalo litawezesha Tanzania kupata vipaji vingi vya wanamichezo kwa watu wenye ulemavu"

Waziri anaendelea na kusema kuwa watu waachane na imani za kishirikina kuwaficha au kuwafungia ndani ndugu zao wenye ulemavu bali wawape uhuru wa kushiriki michezo mbalimbali

Aidha pia Waziri ameitakia kila la heri timu ya Taifa ya Tanzania Tembo Warriors

"Kwa pamoja kama Watanzania tuitakie mema timu yetu ya Taifa Tembo Warriors kwani kama tukifanya hivyo watatuwakilisha vyema na kuchukua ubigwa na kwenda kuipeperusha bendera ya taifa katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 nchini Uturuki" anasema Bashungwa.