Waziri atua Dodoma Jiji
UONGOZI wa Dodoma jiji FC, umesema tayari umekamilisha usajili wa aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Waziri Jonior kuimarisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaoanza Septemb 29, mwaka huu.
Ikumbuke mwanzoni mwa mwezi wa nane Waziri alivunja mkataba wake na klabu ya Yanga baada ya kuitumikia kwa msimu mmoja akitokea Mbao.
Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa Dodoma jiji FC, Fortunatus John alisema usajili wa nyota huyo ni miongoni mwa mapendekezo ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu, Mbwana Makata. Alisema timu iko kambini na itatumia siku 14 watamsiikiliza mwalimu wa kikosi hicho kujua ni idadi ya mechi ngapi za kirafiki anaziitaji ilikujiweka fit na msimu ujao.
“Pia katibu huyo amesema kuelekea msimu ujao 2021/ 2022 wao kama klabu wamempa malengo mwalimu ya kutaka kumaliza katika nafasi 4 za juu kulingana ma usajili walioufanya anaamini malengo yao yatatimia. “ Dodoma Jiji ni miongoni mwa timu zilizosumbua msimu uliopita haswa ikiwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Jamhuri Jijini Dodoma chini ya Kocha Mbwana Makatta.
IMEANDIKWA NA LILIAN MUKULU