Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wazir JR kutimkia Saudi Arabia

MSIBA Pict

Muktasari:

  • Grandez hivi karibuni alikuwa anaifundisha Al Minaa anayoichezea Wazir Jr ambaye mkataba wake wa mkopo unaisha mwishoni mwa msimu.

INAELEZWA Al Faisaly inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Saudia Arabia imemalizana na kocha Mhispania, Pablo Grandez lakini ametoa pendekezo la kuletewa straika Mtanzania, Wazir JR anayekipiga Al Minaa inayoshiriki Ligi Kuu nchini Iraq.

Grandez hivi karibuni alikuwa anaifundisha Al Minaa anayoichezea Wazir Jr ambaye mkataba wake wa mkopo unaisha mwishoni mwa msimu.

Chanzo cha karibu kililiambia Mwanaspoti kuwa kwenye orodha ya wachezaji ambayo kocha huyo anataka kuwa nayo msimu ujao ni pamoja na jina la nyota wa zamani wa Yanga, Dodoma Jiji na KMC, Wazir.

Chanzo kiliongeza kuwa kocha huyo hakudumu muda mrefu wakati Wazir anajiunga akitokea Dodoma Jiji lakini alimtazama mazoezini.

“Wazir ni mshambuliaji wa kati mwenye nguvu na kocha amemuulizia kama hataongeza mkataba mpya na Minaa basi anaweza ajiunge na Faisaly ya Saudia,” kilisema chanzo hicho.

Mbali na ofa ya Saudia Arabia lakini pia Mwanaspoti linafahamu nyota huyo kuna klabu moja kutoka Algeria inamfuatilia.

Wazir Jr ambaye aliwahi kukipiga Yanga msimu wa 2020/21, alijiunga na timu hiyo iliyopo nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi yenye timu 20, kwa mkataba wa miezi sita mwanzoni mwa msimu huu na tangu atambulishwe kikosini hapo Februari 5 mwaka huu, hajapata nafasi ya kuanza moja kwa moja kwenye timu hiyo.