Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watanzania watawala Yas Kili International Half Marathon 2026

LEO Pict

Muktasari:

Katika mbio za Yas Kili Half Marathon kwa mwaka huu, maelfu ya Watanzania wamejitokeza kushiriki huku viwango vya ushindani vikipanda, na ushindi katika makundi mbalimbali ukitawaliwa na wanariadha wa ndani, jambo lililoleta hamasa kubwa miongoni mwa mashabiki.

Leo Machi 22, 2026, Wanariadha wa Kitanzania wameendelea kung’ara katika ardhi ya nyumbani, kupitia mbio za kilomita 21 maarufu ‘Yas Kili International Half Marathon 2026’, huku mwanariadha maarufu Gabriel Geay akishika nafasi ya kwanza.

Mbizo hizi zinazofanyika kila mwaka mkoani Kilimanjaro ni moja ya matukio makubwa ya michezo barani Afrika.

Akizungumza wakati wa kuwapongeza washiriki, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Paul Makonda, amesema mbio za mwaka huu zimeonyesha namna Watanzania wanavyoinuka na kuthibitisha uwezo wao katika riadha.

“Kile kilichofanyika Moshi leo sio tu mashindano; ni uthibitisho wa kujituma, uzalendo na uwezo mkubwa wa Watanzania kushindana na kuibuka na ushindi."

Waziri Makonda pia aliwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameahidi kuwa mgeni rasmi kwa mashindo ya Kili Marathon kwa mwaka ujao huku pia akiahidi kuongeza dau nono la shilingi milioni 100 za Kitanzania kwa washindi.

Yas Kili International Half Marathon imeendelea kuwa jukwaa muhimu linalounganisha watu, kukuza utalii na kuleta hamasa mpya katika sekta ya michezo nchini.”

Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas, Pierre Canton Bacara, alisema ushindani ulioonekana katika mbio za kilomita 21.1 umedhihirisha ubora wa wanariadha wa Tanzania na nguvu ya hamasa inayozidi kukua kila msimu.

Bacara alisema udhamini wa zaidi ya miaka 12 wa kipengele cha Yas Half International Marathon unatokana na dhamira yao kuwa mshirika wa maendeleo ya michezo nchini. Kaulimbiu ya mwaka huu ya “Kila Kona, Kila Hatua Kasi Zaidi,” inaakisi juhudi za kampuni kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia Watanzania kote nchini.

Alisema, “Kwa mwaka wa tatu mfululizo tumetambuliwa na kampuni ya kimataifa ya Ookla kama mtandao wenye kasi zaidi nchini Tanzania. Tunaendelea kuwekeza katika miundombinu ili kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na mawasiliano ya uhakika -iwe ni biashara, elimu, kilimo au kusherehekea mafanikio ya ushindi wa mbio kama hizi za Yas Kili International Half Marathon mtandaoni.”

 “Mwaka huu tunapanda zaidi ya miti 50,000, na jana pekee tuliotesha miche 3,000 katika eneo la Njoro. Huu ni mchango wetu katika kuhakikisha Kilimanjaro inabaki kuwa alama ya fahari ya taifa letu,” alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, aliipongeza Yas kwa kuendeleza urafiki wa muda mrefu na jamii ya mkoa huo na kusema mbio hizo zimekuwa kichocheo cha utalii, biashara na maendeleo ya jamii.

Katika mbio za Yas Kili Half Marathon kwa mwaka huu, maelfu ya Watanzania wamejitokeza kushiriki huku viwango vya ushindani vikipanda, na ushindi katika makundi mbalimbali ukitawaliwa na wanariadha wa ndani, jambo lililoleta hamasa kubwa miongoni mwa mashabiki.

Washindi wa jumla wa Yas Kili International Half Marathon (km 21)  ni;

Wanaume

Michael Geay - (TZ) muda;- 1:04:10

Josephat Joshua Gisumo (TZ) muda 1:04:14

James Kairiuki (KE) muda 1:04:30

Sule Elisante (TZ)

Benard Kiplagat (KE)

Dickson Paul (TZ)

Robert Makenzi(TZ)

Joshua Amos(TZ)

Boniphace Mwangi (KE)

Wanawake

Hamida Musa (TZ)

Failuna Matanga (TZ)

Veronika Wanjiku (KE)

Florence Wachira (KE)

Irene Mkungu (TZ)

Tunu Andrew (TZ)

Leah Bek (Germany)

Leah abeid (Germany)

⁠Everlyne Roytich (UG

 Anisa badalo (TZ