Wataka kuuana kisa maandazi

TIMU ya wafanyakazi wa Gereji na Madogo wa Tabata juzi kidogo wazichape kisa maandazi.
Timu hizo zilikuwa na mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Kigogo na kutoka sare ya bao 2-2 na mwamuzi kumaliza mechi bila ya kuingia matuta.
Mshindi katika mchezo huo alikuwa akijipatia zawadi ya maandazi 60 na baada ya sare wakaahidiana kugawana maandazi 30 kila mmoja lakini Madogo hao wakakataa na kutaka zipigwe penalti hadi apatikane mshindi jambo ambalo Gereji hawakuliafiki.
Baada ya mabishano ya muda mrefu Gereji wakaona isiwe tabu wakakimbia na beseni la maandazi.
“Hawa wamempanga mwamuzi kabisa mechi imeisha kwa sare ilitakiwa kupigwa mikwaju ya penalti lakini haikuwa hivyo kamaliza mechi huyoo kaondoka sio sawa wanataka maandazi tugawane sawa,” alisema Mtaiki mmoja wa madogo wa Tabata.