Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasudan waipora Simba mido wa boli

Muktasari:

  • Awali Simba ndio iliyokuwa  ikiongoza vita hiyo ya kumnasa fundi huyo kutoka ASEC Mimosas, lakini Wasudan hao wameingilia kati dili hilo na kumwaga mkwanja mrefu. Kabla ya Wasudan, Singida Black Stars (zamani Ihefu) ilitajwa pia kumpigia hesabu kumbeba, lakini Al Hilal ikafanya mambo.

MIAMBA ya soka la Sudan, Al Hilal Omdurman imeizidi kete Simba katika mbio za kuwania saini ya kiungo, Serge Pokou aliyekuwa akihusishwa nao katika mpango wa kukiimarisha upya kikosi kipya msimu ujao.

Awali Simba ndio iliyokuwa  ikiongoza vita hiyo ya kumnasa fundi huyo kutoka ASEC Mimosas, lakini Wasudan hao wameingilia kati dili hilo na kumwaga mkwanja mrefu. Kabla ya Wasudan, Singida Black Stars (zamani Ihefu) ilitajwa pia kumpigia hesabu kumbeba, lakini Al Hilal ikafanya mambo.

Simba ilikuwa ikihusishwa na fundi huyo, tangu msimu uliopita na Mwanaspoti iliandika juu ya hesabu ambazo walikuwa nazo Wasudan hao kabla ya kumalizana na mchezaji huyo.

Pokou amejiunga na chama hilo linalonolewa na kocha Mkongomani, Florent Ibenge kwa mkataba wa miaka minne.

Fundi huyo wa Kiavory Coast atatua Tanzania kuungana na wachezaji wenzake ambao wameweka kambi nchini kutokana na michuano maalum inayoendelea kutimua vumbi Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi kutokana na machafuko yaliyopo Sudan.