Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasifu wa kila mgombea Simba huu hapa

Muktasari:

Jumla ya wagombea 18 leo watawania nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu ya Simba katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika kwenye Kituo cha  Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere kilichopo Posta Mpya jijini Dar es Salaam.

WASIFU WA WAGOMBEA SIMBA


MWANAHIBA RICHARD, THOBIAS SEBASTIAN

Jumla ya wagombea 18 leo watawania nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu ya Simba katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika kwenye Kituo cha  Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere kilichopo Posta Mpya jijini Dar es Salaam.
Mgombea mmoja, Swedi Nkwabi atapigiwa kura za ndio au hapana katika nafasi ya uenyekiti wakati wagombea 17 waliobakia watawania nafasi za ujumbe ambazo zitakuwa sita.
Kutokana na umuhimu wa tukio lenyewe, gazeti hili linakuletea dondoo fupi za wasifu wa watu  waliojitokeza kuwania nafasi ndani ya Simba, ambazo  kwa ufupi zitahusu nafasi wanazowania pamoja na  wasifu wao.

1.Swedi Nkwabi-Mwenyekiti

Wasifu. Amezaliwa mwaka 1978 na ana Stashahada ya Juu ya Utawala wa Biashara aliyoipata katika Chuo cha Uhasibu cha CBE.  Amewahi kuongoza nyadhifa mbalimbali katika mpira wa miguu Tanzania, ikiwa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba na kuwa mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanga (TDFA) kwa nyakati tofauti.

2.Patrick Rweyemamu-Ujumbe

Wasifu: Ana shahada ya fedha aliyoipata katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na amehudumu katika mpira wa miguu kwenye nafasi tofauti ikiwemo ukocha wa soka, umeneja wa Simba, Mjumbe wa kamati ya soka la vijana ya Simba na TFF, Mjumbe wa kamati za usajili na ufundi Simba.

 3.Seleman Haroub-Ujumbe

Wasifu: Ana Shahada ya Sayansi ya Jamii na Utawala aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na amehudumu nafasi mbalimbali za michezo ambazo ni mjumbe wa kamati za utendaji KIFA,  Prisons, Mkuu wa Utawala na Michezo kituo cha michezo TAN-ASPO, Mwenyekiti MUFA, Mkurugenzi Mbaspo Academy, mjumbe wa Kamati ya Habari na Masoko TFF na Katibu Mkuu MREFA

4.Jasmine Badour-Ujumbe

Wasifu:Ana elimu ya kidato cha nne aliyoipata katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Sumve na nafasi alizowahi kutumikia kwenye michezo ni Karani Simba, Msimamizi na muanzilishi wa timu ya wanawake ya Simba na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba kuanzia mwaka 2014 hadi sasa.

5. Hussein Kitta-Ujumbe

Wasifu: Ni msomi wa Shahada ya Uzamili ya Sheria aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na nyadhifa alizoshika kwenye soka ni Uenyekiti wa Tawi la Simba Makini, Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa Chama cha Soka Ubungo, Mkurugenzi wa klabu ya Michezo ya Mabomba na Mwanachama wa klabu ya Simba.

6. Christopher Mwansasu-Ujumbe

Wasifu: Ana Shahada ya masuala ya bima na utawala aliyoipata kutoka kwenye Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Nafasi alizowahi kushika kwenye soka ni Mwenyekiti wa Tawi la Kasi ya Simba, Mwenyekiti wa  timu ya New Generation na Mratibu wa vikundi vya michezo na mshauri wa klabu ya Denish  pia kiongozi wa Michezo Shule ya msingi Ikulu.

7.Dk Zawadi Kadunda-Ujumbe

Wasifu: ana shahada ya Uzamivu (Phd) Fedha na Uwekezaji kutoka chuo kikuu ya MSL, India na amekuwa mwanachama wa klabu ya Simba, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Tawi la Simba, Shibam na Ujumbe wa Kamati ya Utendaji na Ufadhili wa Tawi la Simba, Arusha.

8. Said Tully-Ujumbe

Wasifu: Alizaliwa mwaka 1979. Ana Stashahada ya masomo ya Kompyuta na ana uzoefu kwenye soka akiwa kama mchezaji na kiongozi. Amecheza timu za Dar Fire FC, Township Rollers FC, Benki ya Malaysia, Coastal Union na Ashanti United huku kwenye uongozi akishika nyadhifa mbalimbali ambazo ni Mkurugenzi wa Moro United, Mratibu wa Taifa Cup wilaya ya Ilala mwaka 2007/10, Mjumbe wa Kamati za Ufundi na Usajili Simba, Mjumbe wa Kamati ya Soka la Vijana ya TFF na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba.

9.  Hamis Mkoma-Ujumbe

Wasifu: Ana Umri wa miaka 51 akiwa ni msomi wa shahada ya uzamili ya Biashara ya Kimataifa. Ni katibu wa Tawi la Simba Vuvuzela, amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Tawi la Simba Mpira Pesa, Mjumbe Kamati ya Maslahi na Nidhamu za wachezaji Simba na pia Mwenyekiti wa timu ya Mabibo United.

10. Ally  Suru-Ujumbe

Wasifu:Ana Shahada mbili tofauti za uzamili  ambazo ni ile ya Ununuzi na Ugavi aliyoipata katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), na Usimamizi wa Fedha kutoka Chuo cha IFM. Ameongoza michezo katika nafasi tofauti ambazo ni kiongozi wa michezo ya SHIMIWI,  Mjumbe wa Kamati ya Olimpiki, Mjumbe wa kamati ya ;Leseni za Klabu TFF,  Mwenyekiti  Kamati ya Michezo Wizara ya Mifugo na Uvuvi  huku ndani ya Simba akihudumu kama Mjumbe Kamati ya Maendeleo Soka la Vijana, Mjumbe Kamati ya Masoko na Uwekezaji, Mjumbe Kamati ya Fedha, Mjumbe Kamati ya Utendaji na Mjumbe Bodi ya muda ya Wakurugenzi.

11.  Abdallah Migomba-Ujumbe
Wasifu: Ni msoni mwa Shahada ya Utawala wa Utawala wa Biashara aliyoipata katika Chuo  cha Uhasibu (CBE) na uzoefu wake kwenye soka ni kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Tawil la Simba la Ubungo Terminal.

12.Asha Baraka-Ujumbe

Wasifu: Ana shahada ya masuala ya Bima na Biashara aliyoipata nchini England na Mwanachama wa Simba kuanzia mwaka 1984.  Amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ASET inayohusika na masuala ya uandaaji wa matamasha hasa ya muziki.  Amehudumu kama Mkurugenzi wa Bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta kwa miaka 20.

13.Mwina Kaduguda-Ujumbe

Wasifu: Msomi wa Shahada mbili ambazo ni ile Utawala wa Umma na Ushirikiano wa Kimataifa aliyopata katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam lakini pia ana Shahada ya Sheria kutoka katika Chuo Kikuu Huria. Pia ana Stashahada ya Ukocha kutoka katika Chuo Kikuu cha Budapest Hungary. Amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi wa michezo kama vile Katibu Mkuu wa TFF na pia Katibu Mkuu wa Simba ingawa pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).

14. Abubakar Zebo-Ujumbe

Ana Umri wa miaka 43 na ni msomi wa Stashahada ya Juu ya Masuala ya Kuzuia na Kupambana na Ugaidi aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Usalama cha Naif Arab nchini Saudi Arabia. Amewahi Kuwa Katibu Mkuu wa timu ya Polisi Mwanza, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya Chama cha Soka Mwanza (MZFA),  Mjumbe Mwakilishi wa Klabu Mkutano Mkuu wa TFF,  Mlezi wa Matwi ya Simba Chanika na Rock City Fans.