Wapinzani wa Simba AFL kujulikana kesho

Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limetangaza kufanyika droo ya Afrika Football League (AFL) kesho Septemba 2, jijini Cairo, Misri kuanzia saa saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Timu nane pekee zitashiriki mashindano hayo zikiwemo timu zilizofuzu kwa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2023 Al Ahly, Wydad Casablanca, Esperance, Mamelodi Sundowns.
Nyingine zitakazoshiriki ni wawakilishi wa Tanzania Simba SC, TP Mazembe, Enyimba na Petro Atletico.
Ratiba ya mashindano hayo imeundwa kwa misingi ya nyumbani na ugenini. Mashindano hayo yanaanza kwa hatua ya robo fainali na kufuatiwa na nusu fainali kisha fainali.
Mashindano hayo yatafanyika kwa muda wa wiki nne ambapo mechi ya ufunguzi itachezwa Oktoba 20, 2023 katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salam, Tanzania.
Nusu fainali itachezwa kati ya Oktoba 29 na Novemba 1 na mechi za mwisho zitakazoamua mshindi wa AFL kupigwa Novemba 5 na 11 mwaka huu