Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanakimanumanu watambulisha jezi mpya

TIMU ya African Sports ‘Wanakimanumanu’ inayoshiriki Ligi  ya Championships (Daraja la Kwanza) Tanzania Bara leo imetambulisha jezi zake mpya zitakazotumika kwa msimu ujao.

Jezi hizo ni aina tatu kwa maana ya jezi ya nyumbani ambayo ni nyeupe, ugenini (bluu) na jezi ya tatu (nyeusi).

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa timu hiyo, Hatibu Enzi ameeleza kuwa jezi hizo zimedhaminiwa na kampuni ya ulinzi ya K4S Security kwa mkataba wa mwaka mmoja.

“Hizi ndio jezi tutakazotumia msimu huu, ambazo zipo chini ya udhamini wa K4S Security na jukumu zima la jezi tumewakabidhi wao kwa kipindi cha mwaka mmoja,” amesema Enzi.

Pia katika uzinduzi huo walikuepo viongozi kutoka K4S Security, meneja  mkuu, Kemmy Johnson na meneja masoko, Biko Skanda ambao wameeleza kuwa huo ni mwanzo katika nia yao njema ya ‘kuisapoti’ timu hiyo.

“Tumedhamilia kuiunga mkono timu hii kwa mambo mengi, tupo African Sports kama familia na kwa kuanza tumeanzia kwenye jezi lakini mambo mengi mazuri na bora yanakuja,” amesema Biko.

Naye meneja Kemmy amesema; “K4S security tupo hapa kuipa nguvu African Sports na kuhakikisha inarudi Ligi Kuu, pamoja na udhamini wa jezi kwa timu pia tutaipa ulinzi kila mahali itakapokuwa,” amesema.

Pamoja na kutangaza udhamini huo wa jezi lakini pande zote mbili hazijaweka wazi gharama ya udhamini huo.