Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau wataka maboresho mfumo kidigitali

WADAU Pict

Muktasari:

  • Rais (TFF) Wallace Karia Julai 9, 2026 alizindua mfumo huo, aliyosema utasaidia upangaji wa ratiba na kuondoa malalamiko hata ya waamuzi.

BAADA ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) kuzindua mfumo wa kidigitali wa usimamizi wa ligi zote kwa ajili ya msimu ujao wa 2026/27, wadau wameziomba mamlaka hizo kufafanua zaidi ili kujua endapo kukitokea changamoto wanaweza wakatoa maoni wapi na yatafanyiwa kazi muda gani.

Rais (TFF) Wallace Karia Julai 9, 2026 alizindua mfumo huo, aliyosema utasaidia upangaji wa ratiba na kuondoa malalamiko hata ya waamuzi.

“Ni mfumo wa ufuatiliaji wa kidigitali, mfano ratiba ambazo timu zilikuwa zinalalamikia kwamba tumetoka kucheza Mbeya tunaenda Kigoma hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa, angalau kwa wiki zinaweza zikachezwa mechi tatu pia itaondoa malalamiko ya mwamuzi fulani anafuatana sana na timu fulani,” amesema Karia na kuongeza;

WADA 01

“Lakini kuna malalamiko yasiyo na tija ya wachezaji kuchoka, timu tumeziruhusu zisajili wachezaji 40, hivyo niwaombe wasemaji waepuke kuzungumza vitu ambavyo siyo sahihi, ratiba ya ligi itatoka mapema kabla ya Julai 20, Ngao ya Jamii itaanza Agosti 12, ligi itaanza tarehe 14 itaisha Mei 16 2027.”

Katika mahojiano yao na Mwanaspoti wamesema walifuatilia uzinduzi huo kupitia Vyombo vya Habari nchini, hivyo wanaamini ufafanuzi ukitolewa  utawasaidia kuelewa faida zake.

WADA 02

Staa wa zamani wa Simba na Yanga, Said Maulid ‘SMG’ amesema :”Naliona lengo la TFF ni jema kutokana na michuano mbalimbali iliyopo mbele, lakini nilitamani kuwepo na ufafanuzi mfano mtu anataka kutoa maoni yake mitandao itakuwa wazi kuyapokea na yatafanyiwa marekebisho kipindi gani ni katikati ya msimu au mwisho wa msimu.

Ameongeza: “TPLB ina kawaida ya kuwapa nafasi wadau kuchangia maoni yao juu ya kanuni, je, ndivyo itakavyokuwa katika mfumo huo utakuwa na maoni ya wazi kwa wadau.”

WADA 03

Kuhusiana na ligi kuanza Agosti 14 amesema kuna athari ataziona kwa klabu kufanya maandalizi kwa muda mfupi:”Kuna wachezaji wanaweza wakaelewana kwa muda mfupi, kuna ambao itawachukua muda mrefu, wengine wanakuwa na makocha wapya ambapo kila kocha  ana mfumo wake, jambo la msingi ni kujipanga vyema kwa kadri zitakavyoweza.”

Amesema kuhusu timu kusajili wachezaji 40 ni jambo jema, lakini akizitazama Simba na Yanga zenye uwezo na zenyewe zinahesabika wachezaji wenye standadi ya juu pengine wasiozidi 12, hao wengine hawana ulingano wa viwango.

WADA 04

“Kuna tabia za makocha ambao waking’ang’ania kikosi cha kwanza basi kitakuwa hicho hicho, wengine waje wapate nafasi mmoja awe ameumia, kocha pekee tangu nianze kufuatilia mpira aliyekuwa anafanya mabadiliko ya wachezaji na ilikuwa ngumu kumsoma kirahisi ni Nasreddine Nabi hakuwa muoga, ukidhani leo anaingia na kikosi hiki atakushangaza.”

Staa mwingine wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Malimi Busungu amesema: ”Binafsi natamani mfumo huo ufafanuliwe una utofauti gani na uliyopita, faida zake ni zipi, lakini kuhusu muda wa kuanza msimu mpya ni mchache wachezaji wenyewe wanapaswa kujilinda ili kuipa miili nguvu, vinginevyo wengi watastaki mapema sana, kwani watatakiwa kurejea kambini mapema, hivyo wapumzike vya kutosha ingawa wapo ambao maisha yao bila mazoezi hayaendi hao hawana shida.”

WADA 05

Kwa upande wa kipa wa zamani wa Simba na Yanga, Said Mohamed amesema:”Kikubwa wachezaji wanatakiwa kujilinda wenyewe kuendana na ratiba ilivyo, vinginevyo wanaweza wakarejea wakiwa hawajapumzika vizuri, kuhusu mfumo nadhani ni kueleweshwa zaidi, ziwezi kutoa maoni kabla ya kuelewa kiundani jinsi ambavyo utaleta tofauti na ilivyokuwa awali.”

Kwa upande wa mchezaji aliyeshuka na KMC, Darueshi Saliboko aliyemaliza na mabao matano amesema: ”Kwa muda ambao unaanza ligi hapo ni sisi wenyewe wachezaji kujitunza na kupumzika vizuri, ili kujiandaa na majukumu ya msimu mpya.”