Waamuzi walioboronga Simba, Yanga wala umeme
BAADA ya malalamiko mitandaoni kuhusu waamuzi kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara waamuzi wa mechi za mbili za Yanga, Simba wamepigwa umeme.
Mwamuzi wa kati Hussein Athuman kutoka Katavi na mwamuzi msaidizi namba mbili, Godfrey Msakila wa Geita wameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitatu kwa kosa la kushindwa kutafsiri vyema sheria za mpira wa miguu kwenye mechi ya Yanga dhidi ya Mbeya City Februari, 5.
"Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Sh1 milioni kwa kosa la mashabiki wake kuwarushia chupa za maji waamuzi wakiwa wakiwa wanaenda vyumba vya kubadilishia nguo mara baada ya mechi ya Yanga vs Mbeya City uwanja wa Mkapa," imeeleza taarifa ya Bodi ya Ligi.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa beki wa Yanga, Dickson Job amefungiwa na kutozwa faini ya Sh500,000 kwa kosa la kumkanyaga mchezaji wa Mbeya City, Richard Ng'odya jambo lililotafsiriwa ni kuwa mchezo wa hatari.
Katika mechi ya Simba dhidi ya Tanzania Prisons iliyomalizika kwa Simba kushinda bao 1-0, mwamuzi Ahmada Simba wa Kagera ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitatu kwa kosa la kushindwa kutafsiri vyema sheria za mpira wa miguu.