Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana 10 waonwa na Cambinasso kliniki ya kusaka vipaji Moro

Vijana 1680 katika Manispaa ya Morogoro na vitongoji vyake wamejitokeza kwa kujiandikisha kuingia katika programu ya kliniki ya soka ya kusaka vijana wenye vipaji vya soka ili kujiunga katika kituo cha michezo cha Cambiasso cha jijini Dar es Salaam ambako wataendelezwa vipaji vyao ambyo imefanyika katika uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili mkoani hapa, Kocha mkuu wa kituo cha michezo cha Cambiasso cha jijini Dar es Salaam, Meck Mexime alisema mwitikio ulikuwa mkubwa ndani ya siku tatu kwa kukutana na vijana 1680 katika kliniki ya kusaka vipaji vya soka.

Mexime alisema vijana hao wamejitokeza na kucheza soka huku jopo la timu la makocha kutoka kituo cha Cambiasso wakiwa na kazi ya kupenyeza jicho kuangalia mtoto mmoja baada ya mwingine katika kipindi chote ambapo vijana 10 wameonwa na wataingia katika mchujo wa mwisho utaofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

“Vijana 1680 kutoka katika vituo 38 vya kuendeleza vipaji vya soka na wale wa mtaani wamejitokeza katika kliniki yetu ya siku tatu ambapo leo (Juni 23) tumehitimisha kwa kupata vijana 10 ambao wao wameingia katika mchujowa mwisho utaofanyika Dar es Salaam.”alisema Mexime.

Afisa habari wa Cambiasso, Fatuma Nkullo alisema kuwa baada ya kituo hicho kuzinduliwa, Morogoro imekuwa mkoa wa kwanza katika program ya kuendesha kliniki ya kusaka vijana wenye uwezo mkubwa wa kucheza soka na wataonwa na jopo la makocha wa kituo hicho watachaguliwa kujiunga na kituo kuendeleza soka lao.

“Vijana 1680 wamejitokeza katika kliniki ya kwanza kabisa mkoa wa Morogoro ambapo kati ya vijana hao 1680 walipatikana vijana 26 ambao walicheza na vijana wetu wa Cambiasso na kati ya hao 26 vijana 10 ndio walionekana kuwa na uwezo zaidi ya wenzao.”alisema Fatuma.

Fatuma alisema kuwa baada ya kumalizika kwa kliniki ya Morogoro wataelekea Iringa na Dodoma kisha baadaye watafanya kliniki kama hiyo katika mikoa ya Mbeya, Mtwara, Mwanza, Geita,Kigoma na Tanga.

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Reli, Omari Mkesa alisema kuwa utaratibu ulioanzishwa na Cambiasso utaleta tija katika taifa na kuwa Morogoro vijana zaidi ya 1500 wamejitokeza na vijana wenye vipaji wapo wengi.

Mkesa alisema kuwa ni imani yake vijana 10 waliochaguliwa watafuzu na kujiunga na Cambiasso katika safari ya maisha ya soka.

“Morogoro umebahatika kuwa na vijana wengi wenye vipaji vya soka, hii imedhihirisha vijana 1680 wamejitokeza ndani ya siku tatu pekee na endapo ingeongezwa siku ingevuka idadi na kuna vijana ambao hawafikiwa na walimu wenye jicho la utambuzi wa kuona mtoto yupi ana kipaji ama laah hasa katika wilaya za mkoa wetu.” alisema Mkesa.