Vigoma vyatawala kwa Mkapa

Saturday August 06 2022
vigoma pic
By Eliya Solomon

AMAKWELI Wananchi hawana jambo dogo, mashabiki wa Yanga wanaonekana kuwa na vaibu kama lote hapa uwanja wa Mkapa.

Ikiwa ni kilele cha Wiki ya Mwananchi mashabiki hao wa Yanga wameonekana kukoshwa na kufurahia ngoma mbalimbali ambazo zimekuwa zikipigwa nje ya dimba hilo.

Makundi tofauti ya Yanga yameonekana kuja uwanjani kistaili yake, waliovutia zaidi ni wale ambao walikuwa na ngoma kiasi cha kushawishi wengine kujumuika nao licha ya jua la mchana kuwaka.

Hakuna ambaye alikuwa akishikwa mkono kuingia kuselebuka ni mapenzi tu na klabu hiyo, wapo ambao walionekana mzuka kuwapanda zaidi na kuvua mashati.

Nje ya uwanja kuko bize, haraka mbalimbali zinaendelea ikiwa ni pamoja na zoezi la uingiaji ndani

Advertisement