VIDEO: Yacouba arejea nchini, daktari afunguka

Thursday November 18 2021
yakuba pic
By Khatimu Naheka
By Loveness Bernard

Yacouba amerejea akiwa na daktari wa viungo wa Yanga Youssef Mohamed ambaye aliongozana naye katika safari hiyo katika upasuaji uliosimamiwa na daktari bingwa Dahmane Jaleleddine.

Mara baada ya kuwasili Mohamed amesema kila kitu kimekwenda sawa katika matibabu ya Ycaouba na kwamba amerejea kuendelea kupata uponaji akiwa hapa nchini.

Mohamed amesema ingawa mshambuliaji huyo amerejea lakini ataendelea kuwa katika uangalizi mkubwa ambao umetakia kuzingatiwa na daktari Jaleleddine.

"Tumerejea salama baada ya kila kitu kwenda vizuri katika matibabu ya kule Tunisia,sasa anarudi kuendelea na uponaji akiwa hapa hapa nchini," amesema Youssef


"Lilikuwa  ni zoezi lililofanyika kwa mafanikio na kila kitu kilikwenda sawasawa unajua profesa Profesa Jaleleddine (Dahmane) ni mkongwe katika matibabu haya ya magoti na amekuwa akiwatibu wachezaji wengi wa Afrika Kaskazini.

Advertisement


Advertisement