Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Vanessa Mdee abuni viatu vya shule

Muktasari:

  • Mbali na muziki, Vanessa Mdee amekuwa akijihusisha na kampeni mbalimbali za kijamii hasa zile za kuhimiza ustawi na maendeleo ya wanawake hasa watoto wa kike.

Dar es Salaam. Mwanamuziki Vanessa Mdee leo amezindua bidhaa ya viatu vya kike iitwayo 'Bora Star' ambavyo vimelenga kusaidia wanafunzi na watoto wa kike nchini.


Akizungumza katika uzinduzi huo, Mdee alisema wazo la kubuni bidhaa hiyo ni kuwasaidia mabinti hasa wanafunzi wa kike.


"Hii ni moja ya harakati ambazo tumekuwa tukizifanya kwa ajili ya kuboresha maisha ya mtoto wa Kitanzania hasa wa kike. Isitoshe mimi mwenyewe ni binti wa Kitanzania.

“Maisha ni safari ya hatua nyingi. Kwa hiyo naamini hii ni sehemu ya hatua ambayo nimepiga katika kuboresha maisha ya mtoto wa kike," alisema Mdee.


Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Bora Tanzania ambao ndio watengenezaji viatu hivyo, Celline Nyembo alisema watahakikisha vinapatikana katika maeneo mengi nchini.
"Kiatu hiki kitauzwa kwa bei ya Shilingi 35,000 na kitauzwa katika matawi yote ya Kampuni ya Bora hapa Dar es Salaam, Kahama na Arusha.