VIDEO: Mashine mpya za Taifa Stars
Muktasari:
Katika nafasi hizo amewaongeza Aaron Kalambo(Tanzania Prison),Metacha Mnata (Mbao) na Suleman Salula (Malindi Fc Zanzibar). Huku katika upande wa mabeki akiwaongeza Vicent Philipo (Mbao Fc) na Kennedy Wilson (Singida Utd).
KOCHA mkuu wa Timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars', Emmanuel Amunike amekitaja kikosi cha wachezaji 25 kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Uganda. Stars inajiandaa na mchezo dhidi ya Uganda wa kufuzu mashindano ya Afrika, mchezo utakaopigwa 24 March katika uwanja wa Taifa.
Katika kikosi hiko Amunike amefanya mabadiliko kwa kuwatoa nyota waliokuwa katika kikosi hiko na kuingiza wengine ili kuweza Amunike amemuondoa kikosini Beno Kakolanya ambaye yupo nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana kuwa katika sintofahamu na klabu yake, lakini pia amemuondoa Abdi Banda, Ibrahim Ajib na Erasto Nyoni anayesumbuliwa na majeraha.
Katika nafasi hizo amewaongeza Aaron Kalambo(Tanzania Prison),Metacha Mnata (Mbao) na Suleman Salula (Malindi Fc Zanzibar). Huku katika upande wa mabeki akiwaongeza Vicent Philipo (Mbao Fc) na Kennedy Wilson (Singida Utd).
Kikosi kilichoitwa Aish Manula (Simba), Metacha Mnata (Mbao Fc), Suleman Salula (Malindi Fc), Hassan Kessy (Nkana, Zambia), Vicent Philipo (Mbao Fc) , Gadiel Michael (Yanga), Ally Mtoni (Lipuli), Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Andrew Vicent (Yanga), Kennedy Wilson (Singida), Himid Mao (Petrojet) Mudathir Yahya (Azam), Feisal Salum (Yanga), Yahya Zayd (Ismaily), Jonas Mkude (Simba) na Washambuliaji Mbwana Samatta (Genk), Thomas Ulimwengu (Al Hilal), Farid Mussa na Shaban Chilunda (Tenerife), John Bocco (Simba), Shiza Ramadhan (Ennpi), Rashid Mandawa(Bdf) na Simon Msuva (Al Jadida).