VIDEO: Mashabiki Simba watinga maduka ya Vunjabei kusubiri jezi za Simba

MASHABIKI wa klabu ya Simba wamekutana na wakati mgumu baada ya kufika katika duka la VunjaBei eneo la Sinza, Madukani na kukuta pamefungwa.

#LIVE: JEZI mpya za Simba zazua utata kwa Vunja Bei , mashabiki waandamana dukani

Mashabiki hao walionekana kukerwa na kitendo cha duka hilo kufungwa na walipoona waandishi wa habari walisikika wakisema; ”Tuna mengi ya kusema bora mmekuja,”

Wakati mashabiki hao wakiwa wamekaa kwa wingi nje askari wa Jeshi la Polisi nao walikuwa wanaangalia usalama wakiwa na gari mbili aina ya Land Cruiser.

Mashabiki hao baadae walianza kuimba ; ”Hatumtaki Vunja Bei, Hatumtaki VunjaBei.”


AMBULANCE YAKIMBIZWA
Wakati dula la Vunjabei likiwa  limefungwa kwa pembeni kulikuwa na gari la wagonjwa na mashabiki waliwaambia mapolisi kwamba gari hiyo linauza jezi kwa gharama ya juu.

Gari hilo la wagonjwa liliposhtuka dereva wake aliwasha na kulikimbiza ilifanya mapolisi wawashe gari lao moja na kuanza kumkimbiza.

Tukio hilo lilikuwa kama muvi katika eneo hili la Sinza Madukani.