Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VICHAPO : Robben atoa sababu Bayern kuvurunda hasa mwezi aprili

Muktasari:

  • Wakati wote kunakuwa na ugumu kuivunja safu ya ulinzi ya timu hiyo na hata staili ya uchezaji kukabiliana na mazingira hayo inasumbua kiakili.

TOLEO lililopita kwenye Kitabu cha Pep Confidential, Mwandishi, Marti Perarnau aliendelea na mazungumzo na Arjen Robben kubwa walilojadili ni jinsi mchezaji huyo alivyomchukulia Kocha, Pep Guardiola kuhusu staili yake ya uchezaji na kama wangeweza kufanya kazi pamoja na kukubaliana. Sasa endelea…

“Miezi michache ya kwanza wakati wote ni migumu, kunakuwa na utaratibu wa kujenga mazoea taratibu kwa kila mmoja, lakini taratibu tuliendelea kuongezeka ubora kila wiki, kila mwezi na kucheza kwa kiwango cha juu kama ilivyokuwa katika mechi dhidi ya Man City.

“Naipenda staili hii ya soka kwa sababu kidogo inanikumbusha utamaduni wa soka la Waholanzi, soka ambalo Van Gaal alilicheza, kuna kitu katika hilo, staili ya kushambulia, kucheza mpira eneo la mbele bila kubanwa na mabeki, nililipenda kuanzia siku ya kwanza.

Perarnau: “Kushambulia na kukaa sana na mpira eneo la goli la timu pinzani siku hizi si kitu kinachofanyika sana na timu nyingi zinapenda kujazana kwenye ulinzi na kukusubiri uwashambulie.

Wakati wote kunakuwa na ugumu kuivunja safu ya ulinzi ya timu hiyo na hata staili ya uchezaji kukabiliana na mazingira hayo inasumbua kiakili.

Robben: “Ni rahisi kukaba kuliko kushambulia lakini kama unapenda kuwa na mpira ni lazima ufanye jitihada za kutafuta njia nyingine ya kuwashambulia na kujenga kitu kwa kawaida ni rahisi kuliko kubomoa.

“Ni jana tu jamaa alituambia, ukiwa mwanasoka maana yake unafurahia kucheza aina hii ya soka na staili yetu ya uchezaji inakidhi mambo mengi, ingawa nikiri kwenda mbele kushambulia dhidi ya timu yenye kupenda kujihami ni jambo gumu zaidi na zaidi.

Perarnau: “Je, unashangaa wewe ndiye uliyefunga mabao mengi na kutoa pasi nyingi za mabao katika msimu? Je, hilo lina uhusiano wowote na staili mpya ya uchezaji?

Robben: “Nadhani ni hivyo, kuna wakati, Pep aliniambia nisiweke nguvu nyingi katika kuhakikisha napata mabao, aliniambia kama nitaendelea kucheza soka langu mabao yatapatikana hapo hapo na hakika hivyo ndivyo ilivyokuwa.

“Ukiweka umakini katika uchezaji wako, unatafuta vyumba, miliki mpira na kufanya kazi pamoja na wachezaji wenzako hapo wakati wote unakuwa kama tayari umeshapata goli, nafikiri katika hali hiyo hiyo mwisho wa siku nakuwa katika nafasi ya kufunga, kama unakuwa na mpira muda mrefu na unakuwa katikati ya matukio wakati wote unapata nafasi ya kufunga goli.

Perarnau: “Timu ilicheza vizuri Februari na Machi lakini ikaanza kuvurunda Aprili, je, ni aina ya uchezaji au kulikuwa na sababu maalumu na ya kipekee? Vipi kuhusu kubeba taji la ligi mapema, nako pia kulikuwa tatizo?

Robben: “Haikuwa tu kwa sababu tulibeba taji la ligi mapema sana lakini ni vigumu kuelezea nini kingine kilichochangia tatizo, nashindwa kuelewa ni kwanini tuliweza kubeba taji la ligi kwa staili ya aina yake na baadaye kuwa hovyo. Ilikuwa kama vile mambo yalikuwa yakienda hovyo wiki baada ya wiki.

“Kulikuwa na mengi yanayochangia, timu ya soka ina mengi mapana na wakati huo huo yanabadilika kirahisi, mfano angalia namna majanga ya majeruhi yalivyotutesa kwa mwezi Aprili, lakini inanihitaji muda kufanyia tathmini kila kitu na kujua nini hasa kilicho chanzo cha tatizo.

Perarnau: “Timu inaonekana kurudi katika ubora wake, hiyo ni kwa ushahidi wa jinsi mazoezi yanavyokwenda.

Robben: “Ndio hata mimi nafikiria hivyo, tuna nafasi kubwa ya kubeba taji kesho (Kombe la Ujerumani) tofauti na jinsi watu wanavyofikiria, kujiweka katika umakini ni jambo muhimu zaidi na tuko makini kwa asilimia 100.

Perarnau: Pep anasema soka hili ni kama vile linawakilisha mgongano wa kiutamaduni nchini Ujerumani, je, unadhani kweli inaweza kuwa hivyo hapa?

“Robben: Sina shaka na hilo, kila mtu alitambua jinsi tulivyocheza vizuri katika ligi na kumpa Pep heshima anayostahiki lakini mambo ya soka yanahusu matokeo zaidi bila kujali nini tumekifanikisha mwaka huu, pale tu tulipoanza kupoteza mechi pongezi zikapotea na kwa haraka sana tukachukuliwa kama uchafu tu.

“Hata hivyo, ukweli haipo hivyo, tumecheza soka zuri tukiwa na mfumo na tumepata mafanikio makubwa, msimu ujao tunapaswa na tutalazimika kucheza vizuri zaidi, tumeanza kwenda njia sahihi na nasubiri kwa hamu kuianza njia hiyo msimu ujao. Perarnau: “Timu itakuwa bora zaidi kwa sababu umeanza kuuzoea mfumo mpya wa uchezaji?

Robben: “Haswa, mwaka wa kwanza chini ya kocha mpya mwenye staili mpya ulikuwa mgumu na mwaka huu tumeshinda mataji matatu, tumevunja rekodi ya Bundesliga, tumecheza nusu fainali Ligi ya Mabingwa na tunasubiri kubeba Kombe la Ujerumani. Hiyo ni rekodi ya kuvutia kwa mwaka wetu wa kwanza, na sisi wachezaji tunafahamu tunaweza kuwa bora zaidi mwakani kwa sababu tunaelewa kila kitu kwa ubora zaidi.

Itaendelea Jumamosi ijayo…